Pages

Pages

Saturday, January 11, 2014

Mashujaa bendi kukamua wilayani Handeni kesho Jumapili, Ukumbi wa Makuti



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KWA mara ya kwanza tangu kuasisiwa kwake, bendi ya Mashujaa leo inafanya onyesho la aina yake katika Ukumbi wa Makuti, uliopo wilayani Handeni, mkoani Tanga.
Rais wa bendi ya Mashujaa, Chalz Baba, pichani.
Shoo hiyo imekuja katika ziara ya bendi hiyo mkoani Tanga, ambapo Ijumaa walifanya shoo katika Ukumbi wa Mamba Club, uliopo wilayani Korogwe, wakati Jumamosi ya jana walitarajia kufanya shoo Nyumbani Hoteli, Tanga Mjini.

Akizungumza jana kwa njia ya simu leo, Meneja wa bendi hiyo, Martin Sospeter, alisema ziara yao imekuwa na mafanikio makubwa, huku wakiamini kuwa wadau na mashabiki wa Handeni watapata burudani ya aina yake wilayani humo.

“Tunashukuru kwa kupata nafasi ya kufanya shoo wilayani Handeni, hivyo tunaahidi mashabiki wa muziki wa dansi watapata vitu adimu watakapokuja kuangalia kazi nzuri kutoka kwa Mashujaa.

“Mashujaa ni miongoni mwa bendi zenye mguso na nia ya dhati ya kuwa kileleni, hivyo naamini huu ni wakati wetu kudhihirisha makali yetu katika tasnia ya muziki wa dansi hapa nchini,” alisema.

Kwa mujibu wa Sospeter, bendi hiyo imelazimika kukosa nafasi ya kufanya shoo katika jiji la Dar es Salaam, baada ya nafasi tatu za wiki kuanzia Ijumaa hadi Jumapili kuwa katika mkoa wa Tanga, ikisafiri na wanamuziki wake wote, akiwamo Rais wao Charles Gabriel Baba, maarufu kama ‘Chalz Baba’.

No comments:

Post a Comment