Pages

Pages

Thursday, January 23, 2014

Malinzi: Tutaiboresha ligi kuu msimu ujao


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

RAIS wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Jamal Malinzi, amesema msimu ujao wa ligi watakaa ili kuuboresha zaidi, ikiwa ni pamoja na kurudisha mtindo mechi zote za Ligi Kuu kutanguliwa na mechi za vijana.

Rais wa TFF, Jamal Malinzi, pichani.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana Malinzi alisema mtindo utaongeza ufanisi na ushindani katika patashika ya ligi ya Tanzania Bara, huku wakiamini kuwa mpango huo utakuwa na tija kwa sekta ya mpira wa miguu.

Alisema kuwa mara baada ya ligi hii ambayo hatua ya mzunguko wa pili itaanza Jumamosi hii, watakaa na wenzake kulipitisha wazo hilo kwa ajili ya kutafuta fursa ya kukuza mpira wa miguu.

“Tutajaribu kuliangalia wazo la mechi za ligi zote kutanguliwa na mechi za vijana katika viwanja vyote, tukiamini kuwa utakuwa ni mpango mzuri wa kukuza soka la letu, badala ya kusubiri Uhai CUP tu.

“Naamini tutafanikiwa kwa pamoja ukizingatia kwamba tumeingia katika mchakato wa kila mmoja wetu kuhakikisha kuwa anatimiza wajibu wake na kufanikisha maendeleo ya mchezo huo nchini,” alisema.

Malinzi ameingia madarakani katika ofisi za TFF kama rais, akirithi mikoba ya Leodgar Tenga, aliyemaliza muda wake.

No comments:

Post a Comment