Pages

Pages

Friday, January 10, 2014

Coastal Union: Mzunguuko wa pili utakuwa mgumu, tunashukuru kwenda Oman kujiandaa

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WAKATI jana klabu ya Coastal Union ikiondoka nchini kuelekea nchini Oman kwa kambi ya wiki mbili, uongozi wake umesema bila maandalizi ya uhakika timu yao haiwezi kufanya vizuri kutokana na ugumu wa mzunguuko wa pili.
Timu ya Coastal Union wakati wanaondoka jana kuelekea Oman.
Akizungumza jana kabla ya kuelekea Oman, Msemaji wa Coastal Union, Hafidh Kido, alisema kwamba timu zote huwa zinarekebisha makosa yao katika mzunguuko wa pili, hivyo kwao ni changamoto kubwa.
Alisema hali hiyo inawafanya waone umuhimu wa kwenda kuweka kambi nchini humo, wakiamini kuwa itawanoa wachezaji na kuwajenga katika nguvu moja ya ushindi katika mechi za mzunguuko wa pili.
“Ni ngumu timu kufanya vizuri katika mzunguuko wa pili kama hakuna maandalizi ya uhakika, ukizingatia kuwa timu zote zinapania kuziba makosa yao ili wapate matokeo mazuri uwanjani.
Sisi Coastal Union hatukufanya vizuri katika mzunguuko wa pili, hivyo akili zetu zote zipo katika mzunguuko wa pili utakaoanza Januari 25 katika viwanja mbalimbali hapa nchini.

No comments:

Post a Comment