Pages

Pages

Tuesday, January 14, 2014

Coastal kucheza na leo na timu ya daraja la tano leo nchini Oman

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

UONGOZI wa klabu ya Coastal Union yenye maskani yake jijini Tanga kwa Wagosi wa Kaya, umesema kwamba kesho (leo) itacheza mechi ya kirafiki na timu ya Al Seeb SC inayoshiriki Ligi Daraja la tano nchini Oman.
Vijana wa Coastal Union pichani.
Mechi hiyo itakuwa ya pili kwa timu hiyo iliyoweka kambi ya wiki mbili nchini humo kwa ajili ya kujiandaa na patashika ya ligi ya Tanzania Bara, itakayoanza Januari 25 mwaka huu.

Katika taarifa yake iliyotumwa kutoka Oman, Msemaji wa Coastal Union, Hafidh Kido, alisema kuwa mechi hiyo pia ni sehemu ya kuiandaa timu yao yenye mipango kabambe.

Alisema kuwa anaamini wachezaji wao watapata nafasi ya kujiandaa katika mechi zote watakazoingia uwanjani wakiwa nchini humo.

“Tangu tulipowasili nchini Oman tumekuwa tukiendelea na taratibu zetu chini ya benchi la ufundi, ambapo Jumanne tutapata mazoezi tukiwa na wenzetu Al Seeb ya nchini hapa.

“Naamini tutaendelea kujinoa huku wachezaji wetu wakifanyaa bidii kubwa ya kujiweka sawa ili wakifika nyumbani Tanzania wapate mbinu za kufanya vizuri katika mzunguuko wa pili wa ligi,” alisema.

Ligi ya Tanzania Bara hatua ya mzunguuko wa pili inasubiriwa kwa hamu, ambapo timu mbalimbali zimezidi kasi ya kujiandaa, huku Yanga ambao ndio mabingwa watetezi wakijichimbia nchini Uturuki.

No comments:

Post a Comment