Pages

Pages

Sunday, December 22, 2013

Wilaya ya Handeni yafurahia utamaduni kuenziwa

Na Kambi Mbwana, Aliyekuwa Handeni

AFISA Utamaduni wilayani Handeni, mkoani Tanga, Godfray Munga, amesema kwamba kufanyika kwa Tamasha la Utamaduni wilayani humo kumechangia kwa kiasi kikubwa kuitangaza wilaya yao.

Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF Mkoa wa Tanga, Frank Maduga, akiperuzi katika gazeti huku akiwa ni miongoni mwa wadau waliohudhuria tamasha la Handeni Kwetu lililofanyika Jumamosi ya wiki iliyopita, wilayani Handeni, mkoani Tanga.
Tamasha hilo lilifanyika Jumamosi ya Desemba 14 mwaka huu, huku likishirikisha wadau mbalimbali sanjari na viongozi wa serikali, ikiwamo ofisi ya Mkuu wa Wilaya Muhingo Rweyemamu.

Akizungumza mapema wiki hii, Munga alisema akiwa kama Afisa Utamaduni, amefurahi kuona eneo lake la kazi linakusanya watu wengi kwa ajili ya kuenzi jitihada za maendeleo kwa kupitia sekta ya utamaduni.

“Hili ni jambo ambalo limenifanya nione faraja sana katika kuhakikisha kuwa utamaduni wa Mtanzania unaenziwa hususan kwa wakazi na wananchi wa Handeni.

“Naamini mambo yatazidi kuwa mazuri katika siku zijazo kulifanya tamasha lifike mbali zaidi kwa kushirikisha wasanii na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi,” alisema.

Katika Tamasha hilo, mgeni rasmi alikuwa DC Rweyemamu, ambapo alishuhudia umati wa watu ukihudhuria kwa mara ya kwanza na kulifanya kwa mafanikio makubwa.

No comments:

Post a Comment