Pages

Pages

Monday, December 16, 2013

Tamasha la Handeni lafana chini ya udhamini wa NSSF kwa kushuhudia burudani kali za Wazigua na chakula cha asili

Mamia ya wakazi wa wilaya ya Handeni, kutoka katika vijiji vya Kwamsisi,Kwachaga, Kwamkonga, Komsala na vijiji vinginevyo wakiandamana kuelekea katika Uwanja wa Azamio ilikofanyika Tamasha la Utamaduni Handeni Mwaka 2013 ilikuwa ni noumaa Sana

Baadhi ya wananchi kutoka katika vijiji mbalimbali vya Wilaya ya Handeni wakiandamana kuelekea katika viwanja vya Azimio, kuhudhuria msimu wa Kwanza wa Tamasha la Utamaduni Handeni Kwetu 2013, Tumethubutu na kufanikiwa tunasonga mbele...

Akizungumza wakati wa kutambulisha wadhamini na wahisani mbalimbali waliofanikisha kufanyika kwa Tamasha hilo, mratibu wa Tamasha la utamaduni Handeni 2013, Kambi Mbwana alisema udhamini wa NSSF ulikuwa mkombozi mkubwa kwao.

“Awali ya yote napenda kutanguliza shukrani zangu zote kwa wahisani
wa tamasha hili, hasa ndugu zetu wa NSSF maana hakika wameonyesha moyo wa uungwana katika kuhakikisha kuwa Handeni Kwetu inazaliwa kwa mafanikio, ukizingatia kuwa tamasha hili limekusanya watu wa aina mbalimbali.

Awali akizungumza baada ya kuzindua Tamasha hilo ambalo lengo lake lilikuwa ni kuwakutanisha watu wa Handeni kusherekea utamaduni wao pamoja na kukumbusha umuhimu wa kujenga Handeni, Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, alisema kwa kuwa na Matamasha kama hayo jamii inaweza kuwa katika nafasi nzuri ya kupata Maendeleo wanayoyataka.

Muhingo alisema ili mafanikio yapatikane katika kila jambo ni lazima watu wa eneo fulani wawe na utayari wa kukutana na kujadili mambo yao kwa sauti kama waratibu wa tamasha hilo walivyofanya.


“Tunajivunia kuwa na vijana wenye mawazo mapana kama haya, naambiwa tamasha hili ni matokeo ya mawazo ya kimaendeleo ya vijana wetu, hongereni sana,” alisema Rweyemamu.


Kwa upande wake, Meneja wa NSSF, mkoani Tanga, Frank Maduga alisema shirika hilo limedhamiria kuendelea kushirikiana na waaandaaji wa tamasha hilo kwa lengo la kuhakikisha Utamaduni wa Mtanzania unatumika kulitangaza Taifa, pamoja na kutumia fursa hiyo kuchangia shughuli za kimaendeleo kwa kutoa elimu ya huduma zao wilayani Handeni na Tanzania kwa ujumla.


"NSSF ni shirika la Watanzania na tumedhamiria kuwapatia huduma bora Watanzania wote, hivyo kila mtu ana haki ya kujiunga na mfuko huu kwa ajili ya kujiwekea mazingira mazuri katika wakati wote wa maisha yake," alisema Maduga.

Katika tamasha hilo,kulikuwa na vionjo mbalimbali vya Utamaduni wa Wanahandeni, ikiwa ni Pamoja na Ngoma za asili kutoka katika Vijiji vya wilaya ya Handeni kama vile, Kweingoma, Kwamatukutu, Kwediamba, Kwachaga pamoja na vikundi vingine vya Handeni Mjini.

Burudani kali na ya kuvutia iliyoonesha asili kamili ya Mtanzania ilitoka kwa Kundi la Sanaa la Jeshi la JKT Mgambo, Azimio Jazz band bila kusahau msanii wa kundi la Fataki, Machenja ambaye alipiga onesho la kukata kiu akiwa na wana okalandima.


Tamasha la Utamaduni Handeni ambalo linafanyika kwa mara ya Kwanza lilidhaminiwa na NSSF, Clouds FM, Vodacom, Plan B, gazeti la Mwananchi, Kajunason Blog, Chichi Local Wear, Katomu Solar specialist, Dullah Tiles and Construction, Anesa Company Limited, Country Business directory, Jiachie Blog na Taifa Letu.com.
MC-Mtata, Mwani De Omar Nyangasa alifanya yake na kuhakikisha msimu wa kwanza wa Tamasha la Utamaduni Handeni linaenda kama lilivyopangwa, Handeni Hoyeeee
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Muhingo Rweyemamu "Bosi wangu" akiwasili katika Viwanja vya Azimio kuzindua msimu wa Kwanza wa Tamasha la Utamaduni Handeni, ilikuwa ni raha sana ndani ya Uwanja, ambapo pia vyakula vya asili vilipatikana kwenye Tamasha hilo..
Dkt. Khalfani Haula, Mkurugenzi wa Handeni anawasalimu...Hamjambo Handeni!!
huyu ndiye Baba mwenye Nyumba, Mkurugenzi wa Mji wa Handeni, Thomas Mzinga

 OCD wa Handeni, Zuberi Chembela naye alikuwepo

Hawa ni wazee wa Kazi, Azimio Jazz Band....Chezea Mayenuu!!
huyu naye na Mashuka yake kama Maasai...mwanaokalandima, Machenje wa fataki alifanya yake kikwetu kwetu
Mtu Nyomi Sana
Nasema msimu wa kwanza Tamasha la utamaduni Handeni mtu Nyomi sana

Ohoo unashangaa nini sasa?? huu ndio utamaduni wenyeywe kutoka kwamsisi
Twende kazi ni ngoma za asili kwa kwenda mbele, hamna Bongo fleva wala Rhumba.....hatariiiiii
Mzee wa Kijiji...Madini iliyopbaki hapa Handeni kwetu
Funga kibwebwe tusakate sasa

No comments:

Post a Comment