Pages

Pages

Saturday, December 21, 2013

Japhet Kaseba aapa kumtungua Alibaba kesho



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BONDIA Japhet Kaseba, amesema uwezo wake ni mkali hivyo anaamini Alibaba Ramadhan hawezi kumletea madhara katika pambano lao litakalofanyika leo katika ukumbi w Friends Corner, Manzese, jijini Dar es Salaam.
Japhet Kaseba, pichani.
Akizungumzia maandalizi yake, Kaseba alisema kuwa ana kiwango cha juu pamoja na pumzi za kucheza na Alibaba katika pambano lisilokuwa la ubingwa.
Alisema kuwa anaamini mashabiki wake watapata burudani kali kutoka kwake, hivyo aliwataka waingie kwa wingi kushuhudia makali yake katika ulimwengu wa masumbwi.
“Uwezo wangu ni mkali na siwezi kufanya makosa dhidi ya Alibaba, hivyo nimeapa lazima nishinde kwa kuhakikisha kuwa natoa kichapo kwa mpinzani wangu,” alisema.
Kaseba aliwahi kutamba pia katika ulimwengu wa mateke, huku akiwa ni Bingwa wa Ngumi za Mateke na kufanikiwa kuitangaza Tanzania nje ya mipaka yake.

No comments:

Post a Comment