Pages

Pages

Sunday, December 22, 2013

Baada ya kupigwa bao 3-1 na Simba jana, Mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji ambeba mgongoni Juma Kaseja



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWENYEKITI wa Yanga, Yusuph Manji, amesema kwamba klabu yao haijamsajili kipa Juma Kaseja ili aweze kuifunga timu ya Simba, badala yake wametaka kuboresha kikosi chao katika michuano ya Kimataifa, ikiwamo ligi ya Mabingwa Afrika.
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji, pichani.
Jana katika mechi yao ya bonanza inayojulikana kama Nani Mtani Jembe, ilimalizika kwa Simba kuwafunga Yanga bao 3-1 na kuwasononesha mashabiki wa jangwani walioamini kuwa kikosi chao ni imara dhidi ya Simba.

Akizungumza leo asubuhi Makao Makuu ya Yanga, Manji alisema kuwa wanaoamini Yanga inastahili kuifunga Simba kwasababu yupo Kaseja langoni hao wanajidanganya, maana si lengo lao.

Alisema Yanga pamoja na benchi lote la ufundi linaamini kwa kuboresha kikosi chao kwa kuwa na wachezaji wazuri ni safari nzuri ya kutafuta heshima Barani Afrika.

“Mpira una matokeo ya kufungwa na kutoka sare au kushinda, hivyo wenzetu Simba jana walituzidi lakini sio sababu ya kushindwa kuisapoti timu yetu katika michezo yake.

"Mimi jana niliinuka kuwahamasisha mashabiki wote tuendelee kuiunga mkono, hivyo yasitokee malalamiko yoyote au wale wanaotaka jamii ielewe kuwa Kaseja si kipa mzuri au alipaswa kukaa langoni na kuisaidia Yanga iibuke na ushindi dhidi ya Simba,” alisema Manji.

Aidha Manji alizungumzia mipango kabambe ya kuhakikisha kuwa klabu yao inafanya vyema katika michuano ya Kimatataifa itakayoanza mapema mwakani.

No comments:

Post a Comment