Pages

Pages

Saturday, November 30, 2013

Waziri Kigoda ateuliwa kuwa Kamanda wa Vijana Mkoa wa Tanga (UVCCM)



Na Mwandishi Wetu, Tanga.
WAZIRI wa Biashara na Viwanda nchini, Dr.Abdalla Kigoda ameteuliwa kuwa kamanda wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Tanga (UVCCM) katika uteuzi ambao ulifanywa na kamati ya utekelezaji Taifa chini ya Mwenyekiti wao Sadifa Juma.
Dkt Abdallah Kigoda, Waziri wa Viwanda na Biashara
Akizungumza jana katika ofisi za Umoja huo mkoani hapa, Mwenyekiti wa Umoja huo, Abdi Makange alisema mchakato huo ulianzia ngazi ya mkoa ambapo wao waliamua kumpendekeza Kigoda na hatimaye kupata baraka kutoka kamati ya utekelezaji na kumuidhinisha kwa kumpitisha.

Makange alisema hatua yao ya kumpendekeza ilitokana na mchango wake mkubwa aliokuwa ukitolewa na kiongozi huo kwa vijana wa mkoa wa Tanga kitendo ambacho kimewapa wigo katika ufanisi wao, huku akiwa ni mbunge wa Handeni.

“Naishukuru sana kamati ya utekelezaji UVCCM Taifa kuridhia mapendekezo hayo na sasa tunakwenda kufungua ukurasa mpya wa mafaniko ndani yetu “Alisema Makange.

Alisema umoja huo unatarajiwa kuandaa taratibu za kumsimika rasmi kiongozi huyo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Handeni mkoani Tanga lengo likiwa ni kuhakikisha wanatimiza malengo yao waliojiwekea.

No comments:

Post a Comment