Pages

Pages

Thursday, November 07, 2013

Rais Kikwete awazodoa Kenya, Uganda na Rwanda na kuwaambia Tanzania haitajiondoa EAC ng'o


Na Rahimu Kambi, Dodoma
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, amewashangaa majirani zake, nchi za Kenya, Uganda na Rwanda kwa kufanya vitendo vinavyoashiria ubinafsi na kuitenga nchi ya Tanzania, bila sababu za msingi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr Jakaya Mrisho Kikwete, pichani.
Rais Kikwete aliyasema hay oleo mjini Dodoma alipokuwa akilihutubia Bunge, ikiwa ni miaka kadhaa tangu alipofanya hivyo mwishoni mwa mwaka 2010 alipozindua Bunge hilo lilipotoka katika Uchaguzi Mkuu.
 
Akizingumza kwa hisia kali, Kikwete alisema kwamba pamoja na nchi hizo kutaka kuitanga nchi yake, ila Tanzania itaendelea kuipenda Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na kamwe haitaweza kuondoka, licha ya dalili za ubinafsi wa Kenya, Uganda na Rwanda kuongezeka.

Rais Kikwete alisema kwamba wao kama wakuu wan chi wamekuwa wakikutana na kubadilisha mawazo ya kuinga jumuiya hiyo, hivyo inashangaza kuona wapo watu wanaotaka kufanya mambo yanayoshangaza kwa mustakabali wan chi za Afrika.

"Inashangaza kama kuna watu wanaona sisi hatufai kuwa kwenye makubaliano ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, ukizingatia kuwa tunatumia gharama kubwa katika bajeti yetu kutenga mambo ya Jumuiya hii.

"Na kama wenzetu kuna kosa tumelifanya, nadhani njia nzuri ingekuwa kuwa wawazi na sio kufanya mambo ambayo si mazuri kwa mustakabali wan chi zetu,” alisema Rais Kikwete na kuongeza Tanzania itaendelea kuwa kwenye jumuiya hiyo na kamwe hawatakuwa tayari kutoka.

Awali Rais Kikwete pia alitumia muda huo kuzungumzia juhudi za kupambana na majangili Tanzania na duniani kote ili kuweka mkakati sahihi wa kuzuia majangili wanaongamiza rasilimali za Tanzania, wakiwamo wanyama aina ya faru na tembo pamoja na mbao.

Pia alizungumzia mchakato wa kuelekea kwenye Katiba Mpya, akisifia taratibu zote zilizotumika hadi kufikia wakati huu ambapo rasimu ya kwanza imepatikana, huku siku chache zijazo wakitarajiwa kupatikana wajumbe wa Bunge la Katiba.

No comments:

Post a Comment