Pages

Pages

Monday, November 11, 2013

Mwimbaji wa taarabu Nyawana Fundikira afariki Dunia leo jijini Dar es Salaam



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
PIGO limetokea katika muziki wa taarabu kufuatia kifo cha mwimbaji wake Nyawana Fundikira aliyefariki leo jijini Dar es Salaam, akisumbuliwa ugonjwa wa malaria uliosababisha kifo chake na kupokewa kwa uchungu na wadau wote.

Marehemu Nyawana Fundikira mamaa Matashtiti enzi za uhai wake, akiwa ndani ya kundi la T-Moto Modern Taarab. Mwimbaji huyu amefariki Dunia leo jijini Dar es Salaam.

Wadau wa taarabu wamepokea kwa masikitiko makubwa kutokana na kifo cha mwanadada huyo aliyeimba wimbo wa Domo la Udaku akiwa na kundi la T-Moto, lililokuwa linamilikiwa na Amin Salmin Amour.


Mume wa marehemu, Kais Mussa Kais alithibitisha kutokea kwa kifo cha mke wake na kusema kuwa msiba huo umekuja, huku ukimuachia majonzi makubwa. 

Taarifa zaidi za msiba huo zitaendelea kuwajia kadri zitakavyoendelea kupatikana, ambapo kwa sasa mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala, jijini Dar es Salaam.




No comments:

Post a Comment