Pages

Pages

Tuesday, November 12, 2013

Masikini Dkt Mvungi, afariki nchini Afrika Kusini alipokwenda kwa matibabu baada ya kuvamiwa na majambazi jijini Dar es Salaam

HABARI zizlizotufikia hivi punde zinasema kuwa aliyekuwa Mgombea Urais mwaka 2010 kwa tiketi ya NCCR Mageuzi, Dkt Dk Sengondo Mvungi amefariki Dunia akiwa nchini Afrika Kusini alipokwenda kwa matibabu, baada ya kuvamiwa na majambazi hivi karibuni.

Mbali na kugombea urais, kabla ya kifo chake, alikuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katibo, ambapo  Dk Mvungi, (pichani) alikuwa akipata matibabu huko Afrika Kusini kwenye Hospitali ya Milpark.

Marehemu alivamiwa na kupigwa mapanga siku chache zilizopita akiwa nyumbani kwake na kuporwa fedha na baadhi ya vitu vingine vya thamani.

Kwa TanzaniaDk Mvungi ni miongoni mwa wataalamu wakubwa wa Katiba na Sheria.

No comments:

Post a Comment