Pages

Pages

Sunday, November 10, 2013

Ligi yampa wazimu Hamis Tambwe


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MPACHIKA mabao mahiri wa timu ya Simba, Hamis Tambwe, amesema amemaliza ligi akiwa na uchungu kwa kushindwa kuonyesha cheche zake alizotarajia katika mzunguuko wa kwanza wa Ligi ya Tanzania Bara.

Akizungumza jijini Dar es Dalaam juzi, Tambwe alisema kuwa alikuwa na hamu ya kuiweka kileleni timu yake kwa kufunga mabao mengi zaidi, ukiacha bao 10 alizofanikiwa.

Alisema jambo hilo linamfanya arudi kwenye mzunguuko wa pili akiwa na uchu wa kuwa kinara wa kupachika mabao katika mechi za mzunguuko wa pili zitakazoanza January mwakani.

“Nimefanya kila niwezalo ili nifunge mabao mengi zaidi uwanjani, lakini nimefanikiwa kupata bao 10 na kufuatiwa na Elius Maguli wa Ruvu Shooting mwenye bao 9.

“Msimu ujao nitakuwa mkali zaidi kwakuwa nitaendelea na mazoezi hata nje ya michuanio ya Ligi, maana sijapenda niwe kinara kwa mabao machache,” alisema Tambwe.

Tambwe ambaye ni raia wa Burundi, ndio anayeangaliwa kwa umakini zaidi na mashabiki wa Simba wakiamini kuwa anaweza kuipaisha klabu yao na hatimae kunyakua ubingwa.

No comments:

Post a Comment