Pages

Pages

Monday, November 04, 2013

Jeshi la Polisi Zanzibar laipongeza timu ya Polisi Pemba


Na Masanja Mabula -Pemba
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Shekhan Mohammed Shekhan amewapongeza wachezaji wa timu ya Polisi inayoshiriki ligi kuu Visiwani hapa kwa kuonyesha nidhamu na kucheza kwa kujituma na kufanikiwa kuchukua alama sita kutoka Kisiwani Pemba .

Akizungumza na msafara wa timu hiyo huko Ofisini kwake Wete , Kamanda Shekhan amewataka wachezaji na viongozi wa timu hiyo kuongeza juhudi za mazoezi ili kuiwezesha timu kuchukua moja ya nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi na kuiwakilisha Nchi kwenye michuano ya Kimataifa . 

Amesema kuwa bila ya kuwepo na ushirikiano wa dhati  kati ya wachezaji na viongozi pamoja na   kuthaminiana kwa kila mmoja  wawapo nje na ndani ya uwanja mafanikio hayawezi kupatikana .

"Ni jambo la kujivunia kwamba timu umekuja Pemba na kuondoka na alama zote sita , nawaombeni muendelee kushirikiana , kuthaminana na kupendana ndani na nje ya uwanja ili muweze kuiletea mafanikio timu na jeshi la Polisi Visiwani hapa," alieleza Shekhan .

Naye msemaji wa timu hiyo Ramadhan Khamis Ramadhaman amesema kuwa ushindi walioupata kwa mechi za Pemba  umetokana na ushirikiano walionao wachezajio pamoja na Benchi zima la uongozi ambapo kila upande ulitimiza wajibu wake kama ilivyotakiwa.

"Unajua mafanikio haya yametokana na sisi kuwa na ushirikiano, ambapo wachehzaji walitekeleza majukumu yao kama walivyoelekezwa na viongozi nao waliwajibika kwa mujibu na kazi zao," alifamaisha.

Aidha Nahodha wa timu Adam Juma amesema kuwa lengo lao ni kutwa ubingwa wa ligi kuu ya Zanzibar  na kuwataka mashabiki na wapenzi wa timu hiyo kuendelea kuwaunga mkono ili waweze kutimiza azma yao hiyo .

"Lengo ni kuwa mabingwa tumewahi kutwa ubingwa  wa ligi kuu  Zanzibar na tunajua utamu wa ubingwa , sisi wachezaji tumewasha moto na kwa sasa sifikirii kama kuna timu utauzima , tunataka kurejesha heshima na hadhi ya timu yetu,"alijinadi Adam .

Ikiwa kisiwani Pemba Timu ya Polisi imecheza michezo miwili ambapo iliifunga timu ya Kizimgbani Unioted mabao 3-1 kabla ya kuifunga timu ya Jamhuri ambayo inahemea chumba cha wagonjwa mahtuti kwa jumla ya mabao 2-1. na kuifanya timu ya Polis kufikisha alama 19 .

No comments:

Post a Comment