Pages

Pages

Saturday, November 02, 2013

Hafidh Kido apewa usemaji Coastal Union ya Tanga baada ya Edo Kumwembe kujiweka kando



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWANDISHI na mdau wa karibu mno na timu ya Coastal Union ya jijini Tanga, Hafidh Kido, amefanikiwa kurithi mikoba ya msemaji wa zamani Edo Kumwembe kwa ajili ya kazi ya kupashana habari zinazoihusu klabu hiyo.
Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Raia Mwema sasa ndio msemaji mpya wa Coastal Union baada ya Edo Kumwembe.

Akizungumza jana kwa njia ya simu akitokea mkoani Tanga, Mwenyekiti wa Coastal Union, Hemed Aurora, alisema kuwa wamefikia uamuzi huo kwa ajili ya kuiweka nafasi hiyo kwa mtu makini na mwenye kuimudu zaidi.
Edo Kumwembe, pichani.
Alisema kuwa Kido alikuwa mdau wa Coastal huku akifanya kazi kwa karibu na Kumwembe wakati ni msemaji wa klabu hiyo, hivyo wanaamini kuwa atafanya kazi zake kwa moyo naa ujasili wa aina yake.

“Tumeamua kumpa rasmi Kido ili awe msemaji wa klabu yetu akirithi mikoba ya Kumwembe ambaye kwa sasa sio msemaji, huku tukiamini kuwa atafanya kazi zake kwa kujituma kama alivyofanya wakati wote.

“Amekuwa mtu muhimu katika timu yetu kwa muda mrefu sasa, hivyo hatuoni sababu ya kumpa nafasi hii kwasababu anaijua vizuri na ni mtu anayejituma wakati wote katika utendaji wake wa kazi, hivyo wadau na mashabiki wampe ushirikiano,” alisema Aurora.

Licha ya kutangazwa kuwa msemaji wa klabu hiyo, Kido alikuwa ndani ya safu za wadau wa klabu hiyo, huku akifanikiwa kuzunguuka nayo kila mkoa kwa ajili ya kazi ya kupashana habari dhidi ya mwenendo wa timu hiyo ambayo leo inacheza na Mgambo Shooting katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

No comments:

Post a Comment