Pages

Pages

Sunday, November 17, 2013

Coastal B yajipanga kwa Uhai Cup



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

TIMU ya vijana ya Coastal Union yenye maskani yake jijini Tanga, imejipanga vizuri kwa ajili ya kunyakua ubingwa wa mashindano ya Uhai Cup yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Jumapili hii katika Uwanja wa Karume, jijini Dar es Salaam na kushirikisha timu mbalimbali za vijana.

Akizungumza jana kwa njia ya simu akitokea mkoani Tanga, Meneja wa timu hiyo, Abdul Ubinde, alisema kwamba vijana wake wapo sawa kwa ajili ya kuingia uwanjani kumenyana na Azam FC, katika mchezo wao wa ufunguzi.

Alisema kuwa Coastal wanaendelea na mazoezi yao huku wakijipanga vizuri kuhakikisha wanaibuka na ushindi kwa kila timu watakayokutana nayo katika mashindano hayo.

“Mwaka jana tuliingia uwanjani katika mashindano hayo lakini kwa bahati mbaya tuliambulia nafasi ya pili nyuma ya Azam waliyonyakua ubingwa huo, hivyo mwaka huu tumejipanga imara kufanya vizuri zaidi na kushinda kila mechi.

“Naamini kwa jitihada zetu uongozi na wachezaji tutafanikiwa na kutimiza malengo ya kuleta Kombe hilo jijini Tanga, ukizingatia kuwa tuna vijana imara na wenye vipaji vya aina yake,” alisema Ubinde.

Coastal Union yenye maskani yake jijini Tanga Tanzania, ni miongoni mwa klabu zilizowekeza katika soka la vijana jambo linaloweza kuinua sekta ya mpira wa miguu hapa nchini.

No comments:

Post a Comment