Pages

Pages

Thursday, November 07, 2013

Askari wa kutokomeza ujangili walaumiwa Mpanda


Hapa ndipo wanapoishi watu hawa baada ya nyumba zao kuchomwa moto.

Na Walter Mguluchuma-Kativi yetu
Mpanda
Askari waliokuwa wanafanya operesheni ya kuwasaka majangili waliokuwa wakiongozwa na JWTZ  wamelalamikiwa kwa kuchoma nyumba za wanakijiji cha Kabage Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi na kuwasababishia wananchi wa kijiji hicho kuishi chini ya miti na akina mama kujifungua kabla ya wakati

Mwenyekiti wa Kijiji hicho Maganga Kasope alisema tukio hilo lilitokea hapo Oktoba 28 mwaka huu majira ya saa tano asubuhi na kusababisha zaidi ya kaya mia sita kukosa makazi ya kuishi

Alisema kijiji hicho chenye wakazi zaidi ya elfu kumi ni kijiji halali kwani kalisajiliwa  toka mwaka jana na kupewa usajiri wenye namba za usajiri wa kijiji KT/KIJ/47 hivyo wameshangazwa na wakazi wa kijiji hicho kuchomewa nyumba zao wakati ni kijiji halali


Watoto wakiwa michezoni huku wasijue watalala wapi ukifika usiku .

Ni majonzi makubwa.

Hizi ndizo nyumba zao , wanalala chini ya miti baada ya nyumba zao kuchomwa moto.

Wakazi wa kijiji cha kabage wakihama kijiji hicho baada ya nyumba zao kuchomwa na askari waliokuwa wanafanya oparesheni ya kuwasaka majangili nyumba hizo zilichomwa wiki iliyopita kijijini hapo na kusababisha maelfu ya wanakijiji kuishi chini ya miti.
Mzee na binti yake wakiwa wanaondoka wanaondoka.
Wakina mama wakiwa wanafungasha.
Wakubwa kwa watoto wakiwa wanakihama kijiji hicho.
Wakiendelea kuhama kijijini hapo.
Wakazi wa kijiji cha Kabage wilayani Mpanda Mkoa wa Katavi wakiwa wanaishi chini ya miti na familia zao baada ya nyumba zao kuchomwa moto na askari waliokuwa wanafanya oparesheni majangiri wiki iliyopita jumla ya zaidi ya kaya 500 zilichomewa nyumba kijijini hapo na kuleta malalamiko ya wanakijiji hao kwa kile wanachodai kijiji hicho ni halali na kimesajiliwa kisheria toka mwaka jana na kupewa usajili wenye namba KT/KIJ/47.
Hawana makazi tena hawa.
Mtoto akiwa amelala huku akiwa hana pa kuhifadhiwa ikiwa nyumba yao imechomwa moto.
Mchungaji wa kanisa la PAG wa kijiji cha Mwamkulu Petro Mahenga akimfariji mmoja wa wahanga waliochomewa nyumba zao katika kijiji cha kabage wilayani Mpanda Daudi Belehiwa ambae pia mke wake aitwae Kurwa Elias alijifungua mtoto ambae hajatimiza miezi yake kutokana na kutembea kwa muda mrefu wakati akiwakimbia askari hao hata hivyo mtoto huyo aliezaliwa akiwa na miezi nane alifariki muda mfupi baada ya kuzaliwa.
Vyombo vikiwa havina pa kupelekwa.
Dogo akiwa ameishiwa Nguvu.
 Inasikitisha sana Wanakijiji hawa hawana makazi sasa.
Alisema kuwa katika tukio hilo akina mama watatu ambao walikua wajawazito walilazimika kujifungulia kwenye mbuga za mpunga wakati wakikimbia kuelekea kijiji cha jirani cha mwamkulu kujihifadhi hivyo kutokana kutembea kwa umbali mrefu hivyo ililazimika kujifungulia njiani na kujifungua watoto wakiwa salama

Kwa upande wake mhanga wa tukio hilo  Daudi  Lulehiwa 28  alisema kutokana na tukio hilo iliwalazimu ketembea umbali mrefu kwa ajiri ya kukimbilia katika kijiji cha jirani cha Mwamkulu huku wakiwa wamebeba mizigo yao  na iliwalaziri hata watoto wao wadogo kutembea kwa miguu umbali huo mrefu

Alisema mkewe aitwaye Kulwa Elias 24 ambae alikuwa ni mjamzito wa miezi minane  kutokana na kutembea umbali huu huku akiwa amebeba mizigo  aliweza kujifungua mtoto wa wakike  ambae alikuwa sio ridhiki na alifariki muda mfupi baada ya kujifungulia chini ya mti

Nae mchungaji wa Kanisa la wa Kanisa la P.A.G wa Kijiji cha Mwamkulu Mchungaji Petro  Mahega  alisema toka wahanga hao waliokimbilia kijijini hapo wamekuwa wakiishi kama wanyama wao na familia zao

Alieleza kutokana na wahanga hao kuishi chini ya miti na mbaya zaidi hapo juzi walinyeshewa na mvua ambayo ilinyesha majira ya usiku hivyo ametowa jengo la Kanisa lake igawa ni dogo sana litumike kwa ajiri ya kuwahifadhi wahanga hao

Kwa upande wake mhanga mwingine Malidadi Gwachele 72 ambae anaishi na familia yake ya watu 20 wakiwa chini ya mtu alieleza kuwa  wameanza kuhathirika kwa kupata magonjwa ya kuharisha

Alisema hari hiyo imesababishwa na maji wanayo kunywa na mazingira wanayoishi na hasa watoto wadogo ndio wanao athirika zaidi  za magonjwa hayo
Mdae Masanja  alisema mbali ya kuchomewa nyumba yake pia amepoteza chakula chake ambacho kiliteketea kwa moto baada ya kushindwa kukihamisha kwenye nyumba yake wakati ikiungua

Alisema sasa hivi wanalala nje bila hata kujali jinsia za familia walizo nazo kutokana natukio lenyewe inawalazimu walale hivyo na wamekuwa wakijisaidia kwenye vichaka

Aidha Mhanga Katali Ngeleja  alieleza mbele ya mwandishi wa habari hizi ambae alitembelea eneo hilo kuwa wako watoto wenye umri kati ya miaka saba na nane  walipotezana na familia zao kwa muda wa siku mbili 

Alieleza yupo pia mwenzao mmoja ambae alikuwa anamiliki mashine ya kusanga unga iliteketea kabisa kwa moto ikiwa ndani ya kibanda cha nyumba

No comments:

Post a Comment