Pages

Pages

Wednesday, October 16, 2013

Yanga yapitisha wazo la kupigia kura mpango wa klabu yao kuwa kampuni, kura kuanza kupigwa leo Makao Makuu



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WANACHAMA wa Yanga wameombwa kujitokeza kwa wingi Makao Makuu ya klabu hiyo kuanzia leo Oktoba 16 hadi Novemba 10 kwa ajili ya kupiga kura iwapo wanaafiki Yanga kuwa Kampuni.
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, pichani.
Uamuzi huo ulifikiwa katika Mkutano wa Kawaida wa Wanachama wa Yanga uliofanyika Januari 16 mwaka huu, huku Mwenyekiti kwa niaba ya Kamati ya Utendaji akiwapa Wanachama wafikirie mapendekezo ya klabu yao kuwa Kampuni ama kutokuwa Kampuni kisha kuyawasilisha kwa Katibu Mkuu wao.

Akizungumza mapema leo asubuhi, Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako, aliwataka wanachama wao kuchangamkia fursa hiyo ili suala hilo lifikie hatua nzuri.

“Nachukua nafasi hii kuwaambia Wanachama wa Yanga kuwa kuanzia leo Oktoba 16 hadi Novemba 10 mwaka huu kuwa kutakuwa na sanduku moja (1) hapa klabuni kwa ajili ya kukusanya kura za maoni ya Wanachama ya kuanzisha Kampuni (NDIYO) au kutokuwa Kampuni (HAPANA)

“Kila Mwanachama hai atakuwa na uhuru wa kupiga kura na atalazimika kuja na Kadi yake ambapo itamzuia kupiga kura mara mbili au zaidi,” alisema Mwalusako.

Kwa mujibu wa Mwalusako, zoezi hili ni muhimu kwa ajili ya maendeleo ya Yanga na kuwataka wanachama wote wachangamkie fursa hiyo kwa ajili ya kupiga hatua baada ya kutolewa wazo la Kampuni.

No comments:

Post a Comment