Pages

Pages

Saturday, October 19, 2013

Wakazi wa Mwenge wanapochanganywa na vinyesi kiasi cha kutishia magonjwa ya milipuko

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WAKAZI wa eneo la Mwenge kwa zaidi ya miaka mitano wamekuwa wakilishwa kinyesi kinachotokana na kuzibuka kwa chemba za maji taka zaidi ya nane.

Chemba hizo zimekuwa zikizibuka na kutiririsha maji machafu ya kinyesi na kupita katika makazi ya wananchi wa maeneo hayo jambo ambalo ni hatari kwa afya zao.

Pamoja na jitihada za viongozi wa mitaa kutoa taarifa kwa wahusika hakuna chochote kilichofanyika hadi leo jambo ambalo linatishia kuwepo kwa magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu hasa wakati.

Mtandao huu umekusanya matukio katika picha na video yakionyesha hali ilivyo...endelea kutazama chini ujionee mwenyewe...
 Hizi ni Chemba mbili ambazo zimesha jaa na Kupasuka na kusababisha uharibifu mkubwa wa Mazingira na kuhatarisha afya za wakazi wa eneo hili la Umoja street ambapo sasa panaitwa Kinyesi Street.
 Majani Haya si kwamba yamekuwa Kijani kuna mvua katika kipindi hiki cha Kiangazi lakini ni kwamba Maji machafu yanayo Churuzika kila wakati ndiyo yamesababisha kuwepo kwa hali hii hatarishi
 Unaweza kudhani kwamba kuna watu wanakuja kufanya kazi ya kuzibua hizi Chemba hapa , lakini la hasha zimefunguliwa tuu, hii si chemba ya mtu binafsi lakini ni chemba ya mkondo wa maji Taka.
Hivi ndivyo inavyo onekana Moja ya Chemba katika mtaa huu.. Chemba hii inakaribia kabisa kujaa na ikisha jaa itasababisha Madhara makubwa sana katika eneo hili, Tayari chemba mbili zimesha fumuka,Kama takataka zinavyo onesha kwamba muda wowote zikiziba basi chema hizi zitaachia na kuanza kumwaga maji hayo machafu. hii imepita ukutani kwa mtu mda wowote inafumuka.
 Picha inajileza yenyeww hapa Tazama majani yalivyo stawi vizuri sana, Tazama chemba hii ilivyo kaa muda mrefu mpaka inaelekea Kuoza sasa, ni moja ya chemba ambayo kwanza haina mfuniko jambo ambalo ni hatari, pili ni la maji machafu ambayo yanaweza sababisha magonjwa ya mlipuko. Hii ni chemba sugu
 Hali hii ndiyo iliyo sababisha mtaa huu kuitwa Kinyesi Street, kwa mbali kuna mkazi wa eneo hili anaonekana kuvuka barabara kwa shida sana jambo ambalo linaonesha mtaa mzima hasa eneo hili pamejaa maji taka .
Hii ni Chemba ya Maji Taka ambayo kwa msingi kabisa inamwaga maji mengi sana kwa kai ya ajabu pia , mkondo huu ambao sasa umesemwa mpaka wananchi wameamua kunawa mikono na kukubaliana na mtaa wao kuitwa Kinyesi Street.
 Hili ni eneo Hatari sana Hapa Chemba imefumuka inamwaga maji utazania ni yanatoka katika chanzo cha mto, hali hii ni hatarishi sana
 Hivi ndivyo haya maji yanavyo anza safari yake ya kuelekea huko yaendako
 Picha inaelezea Uhalisia kabisa wa Jambo ... Tazama jinsi majani ya upande kwa kulia yalivyo stawi , tazama ya upande wa kushoto yote ni kutokana na Maji taka.

Mbaya zaidi wakati Chemba moja inatema maji kwa wingi hii ipo Jirani kabisa ambapo ukitazama picha ya kwanza ndipo utaelewa vizuri sana . chemba hizi ni hatari sana na mpaka sasa zimebadili sura ya Mtaa huo.
 Huku Ndiko Maji haya yanapo elekea yametokea katika makazi ya watu na yanaelekea katika Makazi ya watu hasa kwenye mkusanyiko wa watu huku Katika Maghorofa ya Jeshi ...........

 Eneo hili ni Moja ya Chemba ambayo Haijatengenezwa na hakuna mfuniko ipo nyuma ya TRA Mwenge kuna majani haya lakini chini ni Chemba mtu akifanya kosa hapa anazama . Lakini Mamlaka husika inalitambua hili na hakuna anaye fanyia kazi hata kidogo
 Hii ni Chemba ya Pili ambayo nayo inatakiwa kupeleka Maji Baharini ni shimo refu lakini hakuna usalama mfunuiko hakuna hakuna kitu chochote kile.. Miaka inapita Mamlaka husika hakuna anaye hangaika .
 Hii ni Chemba ya Tatu ambayo nayo ipo eneo hilo hilo nyuma ya Jengo la TRA lakini hakuna anaye hangaika kupashughulikia ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa panawekewa Mifuniko
 Hapa ni eneo Sugu ambalo Lipo Jeshini pana Chemba  ambayo ina muda mrefu sana na hakuna anaye hangaika nayo ... Hapo Juu ya majani Pana hiyo Chemba ya Maji Taka
 
 Mtaa Huo na eneo hilo hilo kuna Chemba ingine ambayo nayo imefumuka , kwa mujibu wa wakazi wa eneo hili wanadai chemba hii ina Muda wa zaidi ya Miaka 15
 Mtaa huu ambao umebatizwa jina la Kinyesi Street sasa hapo mbele ni Chemba ingine ambayo ni tofauti na zote za awali nayo imefumuka kwa muda mrefu na hakuna anaye hangaika kuja kufumua na kunyonya maji hayo machafu.
 
 Bado Eneo hilo hilo hii ni Chemba ingine kabisa ambayo nayo imefumuka na kumwaga maji yake barabarani .. Wahusika bado wameulizwa wamesema hawana Taarifa hii.

Uchafu umezagaa eneo hili, Harufu mbaya imeendelea kutoka hapa.. hii ni Chemba nyengine tena katika eneo moja ambayo nayo sasa imepasuka kutokana na kuzidiwa na wahusika kuto lifanyia kazi swala hili...

 Sasa Maji Taka yote kutoka Mitaa yote sasa yanaingia katika Mfereji huu mdogo ambao uliwekwa mahususi kama mvua zikinyesha basi maji yapite hapo lakini sasa maji machafu toka chooni na matumizi ya binadamu ndio yanapita hapa na mbaya zaidi yanapita katika makazi ya watu na kusababisha harufu mbaya na kali.
Picha Mbili za Juu Mtu unaweza ukazania kwamba ni mto unapita hapo tena katika makazi ya watu, la hasha hayo ni maji ambayo ni Kinyesi kutoka chooni.. Mkondo umekosa njia na kuamua kujipitia hapo.. Hali hii imesababisha wananchi wapate shida sana kutokana na harufu mbaya inayo waingilia majumbani mwao kila kukicha.. wamepiga kelele sana lakini hakuna anaye sikiliza kilio chao.
Hapa ni Mlangoni kwa mtu maji haya yanalazimisha Kupita lakini inashindikana sasa yakijaa yanaingia moja kwa moja katika nyumba za watu hali ambayo inaongeza kero zaidi

Habari kamili...
Wakazi wa mwenge mtaa wa umoja karibu kabisa na majengo ya jeshi (JKT) wapo hatarini kupata magojwa ya mlipuko kutokana na mkondo wakupitisha maji taka kujaa na kupasuka  bila mamlaka husika kushughulikia  na hivyo kuwa kero kubwa kwa wananchi wanaoishi katika mazingira hayo.

Mmoja kati ya wananchi wanaoishi katika eneo hilo ambaye hakutaka jina lake kuandikwa, kwa masikitiko makubwa amesema kuwa ni zaidi ya mwezi sasa wamekuwa wakipata adhaa hii ya kujaa na kuziba kwa mikondo ya kupitisha  maji taka bila ya wahusika kuzibua angali wanalipa tozo  za kila mwezi  

“Hali hii ya kujaa na kuzibuka kwa mikondo ya maji taka imekuwa ikitokea mara kwa mara hasa kipindi cha masika na wakati mwingine wakati wa kiangazi jambo lililopelekea hata mtaa huu kubadilishwa jina na kugeuzwa kuwa ni mtaa wa kinyesi”

Wananchi hao wameituhumu mamlaka husika kwa kutokutambua majukumu yao na hivyo kupelekea wananchi hao kuingia gharama mara kwa mara kwa kuamua kuzibua wenyewe kwaajili ya kulinda afya zao.

Wananchi hao wanashindwa kuelewa kwanini mamlaka husika inashindwa kutekeleza majukumu yake na kubaki kuchangisha pesa kwa wananchi wakati mamlaka hizo zina mafungu ya fedha kwaajili ya marekebisho ya miundombinu ya maji taka maarufu kama (service charge)

Pamoja na wananchi hao kufanya jitihada za kuwapata watu wa mamlaka ya maji safi na maji taka DAWASCO lakini juhudi zao ziligonga mwamba baada ya kuambia kuwa ni lazima wachangie fedha ya mafuta kwa sababu gari la mamlaka hiyo halina mafuta.

Hofu kubwa ya wananchi wa maeneo hayo ni mvua, hasa katika wakati huu unaoelekea kwenye kipindi cha mvua za masika ambazo zimekuwa na madhara makubwa kwa upande wa magonjwa ya milipuko kama kipindupindu.


TAZAMA SHUHUDIA VIDEO FUPI HAPA YA MAJI HAYO NA MTAA MPYA WA KINYESI.






No comments:

Post a Comment