Na Kambi Mbwana, Dar
es Salaam
KWA sasa hakuna
kinachojadiliwa kwenye soka la Tanzania, isipokuwa purukushani za Uchaguzi Mkuu
wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), unaotarajiwa kufanyika Oktoba 27 mwaka huu.
Rais wa Shirikisho la Soka nchini TFF, Leodgar Tenga, pichani.
Hakuna anayeweza
kuzungumzia jambo jingine zaidi ya uchaguzi huo, maana ndio wanachoona kinafaa
kwao. Sawa, ila ni vyema mawazo ya uchaguzi huo wa TFF ukaenda sambamba na
malengo ya kuendeleza soka la vijana, hasa wanaoishi vijijini.
Pichani ni mtoto ambaye jina lake halikupatikana mara moja, akionyesha uwezo wa kumiliki mpira.
Nasema hivyo kwasababu vijana wengi wanaoishi vijijini wanakosa mahali sahihi ili waonyeshe vipaji vyao, jambo linalowafanya wengi wao waishie njiani na kuwaua njaa.
Nasema hivyo kwasababu vijana wengi wanaoishi vijijini wanakosa mahali sahihi ili waonyeshe vipaji vyao, jambo linalowafanya wengi wao waishie njiani na kuwaua njaa.
Hii siwezi kuvumilia
na kuna kila sababu ya kuangalia namna gani ya kuibua fursa kwa wanamichezo
wetu na kuweka mikakati kabambe kwa ajili ya kuwapatia mafanikio.
Ni rahisi kusema kuwa
duniani kote watu wenye vipaji na wanaofanya makubwa ni wale wanaotokea katika
familia za kawaida kabisa. Hii ni kwasababu wao hutumia muda mwingi kuendeleza
vipaji vyao ili wajikimu kimaisha.
Ni ngumu mtoto wa
kibosile kuacha usingizi wake ili acheze soka, maana wengi wao wanaona ni kazi
ngumu. Sitaki kusema hakuna watoto wa wakubwa au wanaojiweza kimaisha
wasiocheza soka au ngumi, ila ni namna gani tunaweza kufanya mikakati yenye
kuendeleza nguvu kazi ya wanamichezo wetu.
Ni kutokana na hilo,
najaribu kuangalia jinsi watoto wa masikini wanaoishi maeneo ya vijijini
wanapokosa fursa nzuri kimichezo. TFF kama baba wa soka la Tanzania, wanapaswa kusimamia
vyema sera ya soka la vijana, kwa kuhakikisha kuwa kila wilaya inakuwa na
mashindano ya vijana yenye nguvu na mwamko wa aina yake.
Tukifanya hivyo,
Tanzania tutajiweka katika nafasi nzuri na kuona mwelekeo mzuri wa kukuza soka
la Tanzania. Kuna vyama vya michezo vya wilaya na Mkoa pia.
Hivi visionekane
kwenye Uchaguzi Mkuu wa TFF tu, ila wakati wote wafanye kazi zenye kupigania
maendeleo kwa ujumla. Mpira ni pesa. Watoto wengi wa masikini leo wanatembea
kifua mbele.
Wachezaji kama vile
Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu leo hii wanavuna utajiri mkubwa kutoka klabu
ya TP Mazembe ya nchini Congo, bila kusahau majina mengi yanayotesa katika soka
la Tanzania, kama vile Mrisho Ngassa, Kelvin Yondan, Juma Kaseja na wengineo
waliofanikiwa kwa kiasi kikubwa katika mpira wa miguu.
Ni wakati wetu sasa
kuona mikoani kunaanzishwa ligi zenye ushindani na zinazoweza kukuza na kuibua
ari ya maendeleo ya michezo, hususan mpira wa miguu hapa nchini.
Tusibaki kuangalia
juhudi za timu kubwa tu. Tusiache mawazo yetu yabaki kwa uchaguzi wa TFF au
klabu za Simba, Yanga na Azam pekee. Ili mpira wa miguu usonge mbele ni
kuona vijana wengi wanapata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao.
Kwa siku kadhaa sasa
nimekuwa nikipata maombi ya vijana wanaotaka kuendelezwa kisoka. Hawa wengi wao
wapo katika kata zilizopo kwenye wilaya mbalimbali.
Hii ni kuonyesha
jinsi vijana hao wanavyoishia njiani, maana maombi yao mara kadhaa yanakosa
majibu. Ni ngumu sana, hivyo ni wakati wetu wadau wa michezo, hasa TFF kuweka
sera na kuandaa mashindano ya vijana sehemu mbalimbali za Tanzania.
Kama sio wao kuandaa,
basi wawezeshe na kutoa ruhusa ya mashindano makubwa ya vijana kuandaliwa
katika sehemu za Tanzania, hasa wilayani, maana vipaji vingi vinapotea.
Tukifanya hivyo, hata
soka letu litasonga mbele maana vijana watapata sehemu ya kuonyesha vipaji vyao
na baadaye kusajiliwa na klabu za Tanzania, ikiwa ni njia ya kuichezea Taifa
Stars au kusajiliwa kwenye klabu za Kimataifa na kulipwa fedha nyingi.
Kinyume cha hapo,
tuendelee kupiga soga na kuelekeza mawazo yetu katika Uchaguzi wa TFF kila
unapopiga hodi.
+255712053949
No comments:
Post a Comment