Na Magreth Kinabo, MAELEZO
SERIKALI
imesema kwamba inatarajia kuboresha Teknolojia ya
Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika kila kijiji ili huduma zake ziweze
kuwa karibu na wananchi ili kusaidia kupunguza gharama
wanazozitumia.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (katikati) akiwasili katika
ofisi za Wakala ya Serikali Mtandao zilizopo jengo la TTCL mtaa wa Samora leo
jijini Dar es salaam kwa lengo la kuangalia shughuli za usimamizi wa mifumo na
matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika uendeshaji wa
shughuli za serikali
Aidha
Serikali imeeleza kwamba iteendelea kujenga uwezo wa kiufundi
wa kuweza kuzuia uvujaji wa siri, uhalifu na udhibiti wa
sheria ndani ya vyombo vyake ili taarifa za siri zisiweze kuvuja.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue
wakati alipotembelea ofisi ya Wakala ya Serikali Mtandao(e
GA) jijini Dares Salaam kwa ajili ya kuzungumza na menejimenti na wafanyakazi.
“Leo
nimetembelea ofisi hii. Ni eneo la kipaumbele kwa Serikali kwa
kuongeza matumizi ya TEHAMA kwa Serikali, tija, kasi ya utendaji
kazi na huduma za Serikali. Hivyo sehemu hii ni muhimu ya kuifanya Serikali iwe
karibu na wananchi. Tovuti hii iwe ni dirisha la mwananchi
kutatuliwa shida yake.,”alisema huku akitoa wito kwa wananchi wawe tayari kuitumia.
Balozi
Sefue alisema tatizo la changamoto la TEHAMA
kuhusu uvujaji wa siri lipo dunia nzima hata Marekani
wanakabiliana nalo ,hivyo ufumbuzi wake si kuachana nalo bali
kuzuia uvujaji huo na uhalifu kwa kujenga uwezo wa udhibiti.
“Lazima
kuwe na udhibiti mfano wa kisheria tayari tunayo sheria tutaendelea
kuiboresha kulingana na changamaoto zitakazo kuja,” alisisitiza Balozi Sefue.
Alisema
kupitia TEHAMA wananchi wataweza kupata matibabu au elimu na kulizia
huduma wanazotakiwa kuzipta mfano miradi ya visima vya maji imefikia hatua
zipi.
Aliongeza
kuwa hivi sasa wakala huo unaandaa mifumo ya kuwezesha Wizara, Idara na taasisi
mbalimbali za Serikali kufanya kazi kwa ushirikiano.
Akizungumzia
kuhusu ufikishaji wa huduma katika maeneo ya vijijini, Mtendaji Mkuu wa
(eGA) Dk. Jabiri Bakari alisema watatumia ubunifu ili kuhakikisha huduma ya
TEHAMA inatumika kwenye maeneo hayo mfano kwa kutumia sehemu za mkononi
za kawaida.
Wakala
hiyo ulianzishwa Julai mwaka 2012, ambapo taarifa mbalimbali za Serikali
kutoka Wizara, Idara , wakala na taasisi zake zitapatikana kupitia
mtandao wa wakala hiyo.
No comments:
Post a Comment