Pages

Pages

Saturday, October 12, 2013

Rais Mstaafu Benjamin Mkapa alipozindua kampeni ya 'Tusome Tanzania'

Na Benedict Liwenga-Maelezo, Dar es Salaam.
RAIS Mstaafu Mhe. Benjamini William Mkapa jana alizindua rasmi Kampeni ya “Tusome Tanzania (Let’s read Tanzania Campaign) iliyoandaliwa na wadau mbalimbali nchini wenye lengo la kuwahamasisha vijana wa kitanzania kujijengea utamaduni wa kusoma vitabu mbalimbali.
Rais Mstaafu Mhe. Benjamini William Mkapa ambaye pia ni mgeni rasmi akiwasomea hadithi mbalimbali na kuwauliza maswali mbalimbali watoto ambao ni wanafunzi toka shule mmbalimbali leo katika viwanja vya Makao Makuu ya Maktaba ya Mkoa jijini Dar es Salaam.
Katika uzinduzi huo, Mhe. Mkapa ameipongeza kamati ya wadau waandaaji wa kampeni hiyo kwa kujitoa kwao katika kuhakikisha kuwa watoto wa shule ambao ndiyo taifa la kesho wanapata kujionea wenyewe na anatumaini kuwa watahamasika kupenda kujisomea kwa manufaa ya maisha yao.

“Tabia ya kusoma inamjenga mtu kifikra na kumpa mtu mtazamo”. Alisema Mhe. Mkapa. Mhe. Mkapa ameongeza kuwa kwa kuwa elimu haina mwisho, kusoma ni namna ya kujielimisha siku hadi siku na kufungua mambo mapya yanayoipa akili changamoto, hivyo amewasisitizia vijana wajijengee utamaduni wa kusoma hasa vitabu vya kiswahili na Kiingereza.

“Someni kazi za Shaabani Robert mwandishi mkongwe wa Tanzania,  someni kazi za Mariam Abdallah, Ngugi wa Thio’ngo , Chinua Achebe, Ole Soyinka na .” Alisema Mhe. Mkapa.
Aidha, Mhe. Mkapa ametoarai kwa wadau waandalizi wa kampeni ya “Let’s read Tanzania Campaign”  kuwa zoezi hilo lisiishie hapo bali liwe endelevu na kuwafikia watu wengi na haswa vijana, pia amesisitiza kuwa mtandao wa vitabu uhakikishe vitabu hivi vinafika hadi kwenye shule za vijijini na amehamisisha juu ya ujenzi wa Maktaba na kusaidia kuboresha watoto wetu.

Let’s read Tanzania Campaign ni kampeni iliyoandaliwa na vijana kutoka hasasi mbalimbali lenye lengo la kuwahamasisha vijana wa kitanzania kujijengea utamaduni wa kupenda kusoma vitabu kwa ajili ya kuongeza fikra za vijana na kuwasaidia katika maisha yao.

No comments:

Post a Comment