Pages

Pages

Tuesday, October 29, 2013

Pendo Njau atangaza mahaba kwa masumbwi


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

BONDIA Pendo Njau, amesema kwamba hakuna mchezo mwingine anaopenda zaidi ya masumbwi, jambo linalomfanya aendelee kuwa busy katika kuuweka sawa mwili wake.

PENDO NJAU
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Pendo alisema kuwa jambo hilo linatokana na kuwa na dhamira ya kulinda makali yake katika mchezo wa masumbwi nchini.


Alisema tangu akiwa na umri mdogo aliupenda sana mchezo huo, hivyo anaamini kuwa ndio njia ya kumpatia mafanikio katika masumbwi na kupiga hatua Kimataifa.


“Mchezo wa ngumi ndio niupendao, hivyo ninachofanya kwa sasa ni kuhakikisha kuwa naendelea kufanya mazoezi makali kwa ajili ya kunifikisha hatua ya juu ya zaidi.

“Naamini ndio nafasi ya kunifikisha sehemu ninayohitaji, ukizingatia kuwa nafanya yote haya kwasababu ngumi ndio ajira yangu na naipenda kazi hii,”alisema Pendo.


Pendo ni miongoni mwa mabondia makini na wenye uwezo wa juu kupita kiasi, huku akitokea katika mikono ya Japhet Kaseba, aliyewahi pia kuwa Bingwa wa Dunia wa Kick Boxing.

No comments:

Post a Comment