Pages

Pages

Tuesday, October 22, 2013

Malaika wajinadi kwa mpya mbili



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BENDI ya Malaika inayoongozwa na Rais wake Christian Bellah, jana ilijitambulisha rasmi kwa wanahabari sambamba na kuachia vibao vyao viwili vyenye ubora wa hali ya juu.
Rais wa bendi ya Malaika, Christian Bellah pichani.
Nyimbo hizo ni Mtu wa watu na Nakuhitaji, huku zikionekana kukubaliwa na wengi wakiwamo waandishi waliopata nafasi ya kusikiliza kwa mara ya kwanza.

Akizungumza katika utambulisho huo, Bellah moja ya wanamuziki wenye uwezo wa juu wa kuimba, alisema kuwa mipango yao ni kuwa bendi tishio katika tasnia ya muziki wa dansi hapa nchini.

Alisema kuwa bendi yao imesheheni waimbaji wazuri na wenye kiu ya mafanikio, hivyo anaamini kuwa wote watafanya kazi kwa ushirikiano na kukwea kileleni.

“Hii ni bendi yenye mipango na tunaamini kwa pamoja mashabiki hawatajutia hata kidogo kutuunga mkono maana tupo imara kupita kiasi.

“Tunachopigania kwa sasa ni kuona nyimbo zetu mbili mpya tulizoachia zinawaingia vilivyo wadau wetu, ukizingatia kuwa ndio matarajio yetu,” alisema.

Wengine wanaounda bendi hiyo ni pamoja na Totoo ze Bingwa, Andrew Sekedia, huku ikitarajia kuzindua rasmi bendi yao Novemba 15 katika Ukumbi wa Mzalendo Pub Kijitonyama, jijini Dar es Salaam.


No comments:

Post a Comment