Pages

Pages

Thursday, October 10, 2013

Kwaya ya Kijitonyama kuzindua DVD yao ya 'Namtangaza Kristo' Oktoba 13

Mwenyekiti wa Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama ya Jijini Dar, Emmanuel Shedo maarufu kama 'MC Fomafoma' akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya tamasha la uzinduzi wa CD na DVD yao ambayo inaenda na kwa jina la 'Namtangaza Kristo' ambayo itafanyika tarehe 13/10/2013 kwenye kanisa lao lililopo Kijitonyama, Dar. Kutoka Kulia kwake ni Mwimbaji Modesti Mogani, Mwimbaji na Mtunzi Oliver Israel.
Kutoka Kulia ni Meneja Mipango wa Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama,  Onai Joseph, Mwenyekiti wa Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama, Emanuely Shedo maarufu kama 'MC Fomafoma', Mwimbaji Modesti Mogani, Mwimbaji na Mtunzi Oliver Israel.Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama jijini Dar es Salaam inatarajia kufanya tamasha la uzinduzi wake wa albamu 'Namtangaza Kristo' kwa CD na DVD.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kwaya, Emanuely Shedo alisema nia na madhumuni yao ni kufanya tamsaha la uzinduzi wa kwaya utakaoendana na Jublee.
Aliongeza kuwa siku hiyo kutakuwa na live bendi pamoja na kwaya nyingine ambazo zitaungana nao. DVD na CD zitauzwa siku hiyo pamoja na fulana za 'Namtangaza Kristo' ikiwemo pia Key Holder za Kijitonyama. Msikose watu wote hakuna kiingilio (Itakuwa ni bure kabisa).
Waandishi wa Habari pamoja na wanakwaya wakifuatilia mkutano.
Meneja Mipango wa Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama,  Onai Joseph akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari juu ya uzinduzi wao.
Wanakwaya wa Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama wakitoa burudani mbele ya waandishi wa habari.
Mwimbaji na Mtunzi Oliver Israel (aliyenyoosha mikono) akiongoza kwaya.
Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.

No comments:

Post a Comment