Pages

Pages

Tuesday, October 15, 2013

Kaseba alilia wadhamini wa kuendeleza masumbwi

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

BONDIA wa Ngumi za kulipwa hapa nchini, Japhet Kaseba, amesema kwamba lengo lake la kukuza mchezo wa masumbwi linasua sua kutokana na kukosa wadhamini.

Japhet Kaseba, pichani.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Kaseba alisema kuwa camp yake ya kufanyia mazoezi imesheheni vijana mbalimbali wenye uwezo wa juu, ila wanashindwa kufika mbali kutokana na kukosa dhamira na namna ya kuwaandalia mashindano ya vijana.


Alisema hali hiyo inampa wakati mgumu kuwafanya vijana hao wacheze ngumi kwa mafanikio yao licha ya baadhi yao kuwa na malengo ya kupiga hatua na kuwika.


“Hili ni jambo linalonifanya niumie kichwa kwa kiasi kikubwa mno, ukizingatia kuwa lengo langu ni kuwaandalia mashindano na kuwakusanya vijana wengi zaidi.

“Wengi wanafanya mazoezi, lakini kupanda ulingoni kuonyesha vipaji vyao kunahitaji mashindano au mapambano mengi yanayohitaji pia fedha za kutosha,” alisema.


Kwa mujibu wa Kaseba, vijana wengi wanaofanya mazoezi yake katika kambi yake ya masumbwi, wana vipaji imara, isipokuwa sehemu ya kuonyesha makali yao inakuwa ngumu.


Suala la wadhamini katika mchezo wa masumbwi ni moja ya changamoto kubwa zinazowakumba wadau wa ngumi hasa wale wenye hamu ya kuuendeleza mchezo huo.

No comments:

Post a Comment