Pages

Pages

Sunday, October 20, 2013

Habari zilizotufikia hivi punde zinasema Mtangazaji Julius Nyaisanga amefariki Dunia mkoani Morogoro

HANDENI Kwetu blog imepata taarifa za kushtua katika tasnia ya habari na utangazaji kutokana na habari za kifo cha Mtangazaji mkongwe nchini Tanzania, Julius Nyaisanga, aliyekuwa mfanyakazi wa Abood Media mjini Morogoro.
Habari kutoka kwa mfanyakazi wa redio hiyo ambaye pia hakupenda kutaja jina lake moja kwa moja kwakuwa sio msemaji wa familia wala redio hiyo zilisema kuwa Nyaisanga maarufu kama Uncle J amefariki.
 
Taaarifa zaidi za msiba huo zinaendelea kusakwa hasa kutoka kwa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Morogoro, pamoja na familia yake.

No comments:

Post a Comment