Pages

Pages

Tuesday, October 01, 2013

Extra Bongo wamlilia marehemu Watuguru


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BENDI ya Extra Bongo, imestushwa na kifo cha mpiga gitaa wa bendi ya WK sound, Joseph Watuguru, aliyefariki juzi na kupangwa kuzikwa leo Kongowe jijini Dar es Salaam.
Marehemu Jose Watuguru kushoto enzi za uhai wake.
Watuguru aliwahi kutamba na bendi kadhaa hapa nchini, ikiwamo ile Mchinga Sound akiwa na wakali mbalimbali, hasa Mwinjuma Muumini maarufu kama kocha wa Dunia.
Mkurugenzi wa Extra Bongo, Ally Choki.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa bendi ya Extra Bongo, Ally Choki, alisema kuwa kifo cha Watuguru ni pengo katika tasnia ya muziki wa dansi nchini.

Alisema marehemu alifariki kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya TB, huku akiacha mke na watoto wawili na msiba wake upo nyumbani kwa kaka yake Kongowe.

“Watuguru ni miongoni mwa wanamuziki waliokuwa na uwezo mkubwa hapa nchini, hivyo kifo chake ni pengo katika ramani ya muziki huo na wengi tutamlilia.

“Mpiga gitaa huyo mwenye uwezo wa aina yake amepangwa kuzikwa kesho, hivyo sisi kama Extra Bongo, tumeguswa na msiba wake na hakika tutaendelea kumuombea mema zaidi huko aendako,” alisema.

Mbali na Exta Bongo, wadau na wanamuziki mbalimbali, akiwamo Muumini nao waliguswa na msiba huo kiasi cha kumuongelea marehemu kutokana na kujadili kipaji chake kwenye kona ya muziki.

No comments:

Post a Comment