Pages

Pages

Tuesday, September 10, 2013

Tamasha la Kili Music kufanyika Leaders Club Jumamosi hii kushirikisha wakali kibaoo



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TAMASHA la muziki linalojulikana kama (Kili Music Tour), linaloandaliwa na Kampuni ya Bia ya Kilimanjaro linatarajiwa kufanyika Jumamosi ya Septemba 14 katika Viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam na kushirikisha wakali kibao
Msanii Ney wa Mitego pichani.
Wasanii wanaotarajiwa kutoa shoo katika tamasha hilo ni pamoja na Diamond Platinum, Profesa Jay, Ben Pol, Lady Jay Dee, Linex, Roma, Recho, Kala Jeremia, Joh Makini, Mzee Yusuph, Mashujaa Band, Ney wa Mitego, Ras Six na Tip Top Connection.


Rais wa Manzese, Ahmad Ally 'Madee' pichani
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo na waandishi wa habari, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe, alisema kuwa Tamasha hilo lenye kauli ya mbiu ya ‘Kikwetu Kwetu’, linafanyika huku mipango yote ikiwa imefanikiwa kwa kiasi kikubwa ili kuwapatia burudani wapenzi wao.


Recho wa THT, akiwa jukwaani.
Tukio hilo la aina yake linafanyika ikiwa ni siku chache baada ya kumaliza ziara katika mikoa saba waliyotembelea, wakiwa na wasanii mahiri ambao pia wengi wao ni wale waliofanya vyema katika Tuzo za Kili mwaka huu.


No comments:

Post a Comment