Pages

Pages

Tuesday, September 03, 2013

Simtank yazindua tenki la aina yake na kushangaza wengi

Tenki linakandamizwa huku watu wakishuhudia. Kushoto ni Meneja Mkuu wa SILA AFRICA, Alpesh Patel.

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KAMPUNI ya SILA AFRICA leo imezindua matenki mapya kutoka SIMTANK yenye kiwango cha juu ubora pamoja na uimara wake.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Alpesh Patel alisema matenki hayo yanaweza kukandamizwa bila kupasuka wala kutoboka.
Meneja Mkuu wa SILA AFRICA, wazalishaji wa Simtank, Alpesh Patel akionyesha tenki lililokandamizwa na baadaye kunyooshwa kwa mikono ya binadamu wa kawaida na kukaa sawa. Picha zote na Kambi Mbwana..

Alisema anaamini wateja wao watapata bidhaa bora kutoka kwenye kampuni yao hiyo iliyokuja na jambo linaloshangaza wengi.

“Hili tenki letu linaweza kuanguka kutoka juu kabisa likiwa na maji, lakini haliwezi kupasuka wala kutoboka, hivyo hili si jambo rahisi.

“Endapo limepinda, mtu anaweza kulinyoosha na mambo yakawa sawa, hivyo sisi tunaamini wateja wetu wamepata bidhaa bora,” alisema.

Bidhaa hiyo ilizunduliwa rasmi leo na kila mteja wao anaweza kujipatia huduma nzuri kutoka kwao.

Uzinduzi hapa unafanyika rasmi kabisa. Hao watoto nao walialikwa kushuhudia tukio hilo la aina yake.

No comments:

Post a Comment