Pages

Pages

Sunday, September 01, 2013

Mtoto Salha Ibrahim Mabewa akusanya watu katika HAKIKA yake iliyoambatana na kutimiza siku 40 tangu alipozaliwa

 Watoto hawa wa Madrassa wakipata chai katika HAKIKA ya mtoto Salha Ibrahim Mabewa maeneo ya Magomeni Makuti, jijini Dar es Salaam. Picha zote na Kambi Mbwana.
 Baada ya kisomo kumalizika na mtoto Salha Ibrahim Mabewa kutolewa nje katika shughuli ya HAKIKA yake iliyofanyika leo Magomeni Makuti, jijini Dar es Salaam, watu walianza kugawa chai kama wanavyoonekana hapo waandaazi wakiwa busy kuwalaki wahudhuriaji wao.
Mtoto Salha Ibrahim Mabewa, akitolewa nje katika shughuli ya HAKIKA yake iliyofanyika leo Magomeni Makuti, jijini Dar es Salaam. Aliyembeba ni babu yake aliyejulikana kwa jina la Mzee Rajabu, ambapo pia alitumia fursa hiyo ya kumtembeza kwa wageni waalikwa na wahudhuriaji wa tukio hilo la aina yake kwa mjukuu wake huyo. Handeni  Kwetu Blog inamtakia maisha mema na yenye mafanikio mtoto Salha katika kipindi chote cha uhai wake. Picha zote na Kambi Mbwana.


 Mzee Rajabu akimtembeza mtoto Salha Ibrahim Mabewa kwa wahudhuriaji wa HAKIKA yake iliyofanyika leo Magomeni Makuti, jijini Dar es Salaam.
 Kila mmoja alipata fursa ya kushiriki kwenye tukio hilo la kukumbukwa la mtoto Salha Ibrahim Mabewa.
 Hapa watu wakiwa wamejipanga kwa ajili ya kupata chai. Kilichonivutia zaidi ni huyo mwenye jezi nyekundu kupewa kikombe chekundu. Je, ni mnazi wa Simba? Ninachojua baba shughuli Ibrahim Mabewa ni mnazi wa Yanga. Tena mfurukutwa kabisa. Utamwambia nini kwa Yanga yake? Sasa huyu nahisi atakuwa mtani wake wa jadi.
 Maustadh wakiwa wapo busy na kisomo katika HAKIKA ya mtoto Salha Ibrahim Mabewa, aliyetolewa nje katika shughuli iliyofanyika leo Magomeni Makuti, jijini Dar es Salaam.
 Ibrahim Mabewa aliyekaa kulia na mwenye kofia, akijadili jambo na mgeni wake katika shughuli ya HAKIKA ya mtoto wake Salha, leo Magomeni Makuti, jijini Dar es Salaam.
Ibrahim Mabewa mwenye kanzu akizungumza na wageni wake katika shughuli ya HAKIKA ya mtoto wake Salha, iliyofanyika leo Magomeni Makuti, jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment