Pages

Pages

Saturday, September 07, 2013

KWEINCHILI (2): Tufunge mkanda kwa maendeleo ya Handeni



Na Adam Seif Malinda,     
WIKI iliyopita nilizungunzia umuhimu wa kuunganisha fikra za wana Handeni, ikiwa ni demokrasia ya haki pale inapohitajika kuunganisha watu kutatua jambo fulani, ni vema kila mtu akapata fursa ya kutoa ya moyoni.
                Adam Seif Malinda, mwandishi wa safu hii.
Nilizungunzia uwepo wa ardhi yenye rutuba, isiyohitaji mbolea ya viwandani, uwepo wa madini ya dhahabu, uwepo wa misitu ya asili inayoteketezwa kwa kukata mkaa, bila kuwa na jawabu makini la kutatua kero za umaskini.

Baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alishawahi kusema enzi ya uhai wake kuwa hakuna umasikini mkubwa kama umasikini wa fikra.

Jambo hili ni dhahili tunahitaji kulifikiria mara kadhaa katika vichwa vyetu, kwani naamini wana Handeni hatuna umaskini wa fikra bali tuna umasikini wa kipato ambao tunaweza kupambana nao.

Kila mmoja wetu aliyejiunga katika mtandao wa Handeni kwetu anapaswa kujitathimini anadhani tufanye nini kuibadilisha Handeni kiuchumi, kupitia juhudi zetu wenyewe bila kuingiliwa na wanasiasa ambao wakishirikishwa hawachelewi kuingiza migogoro kwa maslahi ya kisiasa.

Jiografia ya Handeni inafahamika, kuna mabonde mengi yanayofaa kwa kilimo, je juhudi za kuikomboa Handeni kiuchumi tuiielekeze katika kilimo?, kuna madini katika milima iliyoizunguuka Handeni yote na makampuni makubwa yameshaingia, je tuingiuze fikra zetu kwa makampuni hayo yachangie sekta za kijamii katika kuhakikisha madini yanawanufaisha wananchi wa Handeni?, ama tuelekeze wapi?.

Lakini yote haya hayawezi kufanikiwa lazima kuwepo na kikundi kinachotambulika katika serikali yetu, kilichoweka wazi mlengo wake na katiba ambayo inakubalika kisheria, shime tuangalie namna ya kufanya kuunda kundi la ukombozi wa kiuchumi kimawazo na mifano hai ya utekelezaji ili wananchi watuunge mkono, tusiishie kuchati katika mitandao.

Kuna njia nyingi za kufanya kwa kuwa maisha ya kidigitali, muda wa kukutana ana kwa ana ni mdogo tupange muda, tujiunganishe katika kompyuta zetu tufanye mkutano kwa njia ya mtandao, waliopo Uingereza, Japan, Marekani, na kwingineko na sisi tuliopo nchini tujadiliane hatua za kufanya, ili utekelezaji uanze mara moja.

Kwa kuwa wadau wenzetu tunawasiliana kutoka Handeni watueleze ni yapi mageni yanayojili katika kaya zetu tulikotokea ama wengine kuzaliwa, hii itatuwezesha kujenga misingi imara ya kuikomboa Handeni.

Salaam zangu kwenu ni kuwa, kweinchili ni pembeni kidogo ya kitongoji, enzi za wazee wetu ’wahenga’ walikuwa na kimsitu ambacho hutumika kufanya kazi za mikono kama kutengeneza mikuki, tezo, mipini, kunoa visu, mapanga, shoka.
 
 e- mail  adam.seif70@yahoo.com

No comments:

Post a Comment