Pages

Pages

Sunday, September 01, 2013

Kigi Makasi kuwaaga Simba kesho tayari kuelekea nchini India


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MSAKATA kabumbu wa Simba, Kigi Makasi, anatarajia kuwaaga mashabiki wao katika mechi ya kesho dhidi ya Mafunzo ya Zanzibar, mechi itakayopigwa katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Mchezaji wa Simba, Kigi Makasi, pichani.
Makasi anatarajiwa kuondoka Tanzania kuelekea nchini India kwa matibabu yake ya goti baada ya kuumia katika mechi za mzunguuko wa pili msimu uliopita.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Simba, Ezekiel Kamwaga, alisema kuwa mchezaji wao huyo atatumia mechi hiyo kuwaaga mashabiki na wanachama ili wamuombee dua katika safari yake hiyo ya nchini India.

Alisema kuwa maandalizi ya safari yake yamekamilika, huku wakiamini kuwa atakaporudi safari yake atakuwa kwenye kiwango kizuri na mwenye uwezo wa kuitumikia klabu yake ya Simba.

“Makasi ataondoka nchini mapema wiki ijayo kwa ajili ya kuelekea kwenye matitabu nchini India, huku nikiamini kuwa mechi ya Mafunzo itakuwa fursa yake ya kuwaaga mashabiki wa Simba.

“Simba tunamuombea afya njema na safari yake iwe na mafanikio na aweze kurudi salama kwa ajili ya kuwapatia burudani mashabiki wetu,” alisema.

Kwa mujibu wa Kamwaga, safari ya mchezaji huyo kuelekea nchini India imeshakamilika, huku akiitumia mechi hiyo kuwaaga mashabiki na wachezaji wenzake, japo hatakuwapo uwanjani kucheza mechi ya kirafiki na timu ya Mafunzo ya Zanzibar kesho jumatatu.

Mwisho

No comments:

Post a Comment