Pages

Pages

Saturday, September 07, 2013

Jeshi la Polisi wilayani Handeni kutangaza vita ya bange na gongo



Na Kambi Mbwana, Handeni
JESHI la Polisi wilayani Handeni, mkoani Tanga, limesema wilaya hiyo kwa sasa inakabiriwa na changamoto ya matumizi ya bange na gongo, hivyo wanajipanga vilivyo kulidhibiti suala hilo.
OCD wilayani Handeni, mkoani Tanga, Zuberi Chembera, akizungumza jambo na Handeni Kwetu Blog wilayani hapa.

Hayo yalisemwa na Mkuu wa jeshi la Polisi wilayani humo, OCD Zuberi Chembera, alipotakiwa na Handeni Kwetu Blog aelezee hali ya uhalifu katika maeneo yote ya Handeni.

OCD Chembera alisema hali ya uhalifu kwa sasa wilayani humo imepungua kwa kasi na kubakia suala la gongo na bange.

Alisema kutokana na suala hilo, ofisi yake inajipanga imara kuhakikisha kuwa linaondoa kabisa hali hiyo kwa ajili ya kuifanya wilaya hiyo ya aina yake katika mkoa wa Tanga.

“Hakuna matukio makubwa ya uhalifu kwa wilaya hii kutokana na utendaji wa jeshi la Polisi wilayani na Taifa kwa ujumla, hivyo hili tunajivunia na kuwashukuru wananchi.

“Hata hivyo, jukumu letu tuliokuwa nalo ni kudhibiti pia matumizi ya bange na gongo kwasababu hayo ndiyo kero kubwa na lazima tujipange kwa ajili ya kulitokomeza suala hilo,” alisema.

Kwa mujibu wa OCD Chembera, vijana wake wamejipanga imara na kugawana vyema majukumu ya kiutendaji hali inayopunguza matukio ya uhalifu wilayani hapa.

No comments:

Post a Comment