Pages

Pages

Saturday, September 21, 2013

January Makamba apinga kuhusisha siasa na mgogoro wa kiwanda cha chai Bumbuli



Ray Said, Bumbuli
Naibu  Waziri  wa  Mawasiliano  Sayansi na  Teknolojia  January  Makamba  amewataka  baadhi  ya watu  kuondokana  na dhana  ya  kusema  mgogoro  wa  kiwanda cha  chai  cha  Mponde   ni siasa badala  yake amewataka  kuiacha  serikali  indelee na taratibu zake  za  kulitafutia  ufumbuzi  swala hilo. 
Mbunge wa Bumbuli, January Makamba, pichani.
Makamba  ambaye pia ni Mbunge  wa  jimbo  la Bumbuli, alisema lazima ashirikiane na wananchi wake na si kikundi cha watu wachache licha ya kutukanwa kwa kwasababu ya kuwaunga mkono wananchi.

Naibu  waziri huyo alieleza kusikitishwa kwake na baadhi ya watu kuliingiza suala hilo kwenye kisiasa na kwamba lina maslahi binafsi  huku mambo hayo yakiachwa tangu mwaka 2010  baada ya kumalizika uchaguzi, hivyo kwa sasa ni wakati wa kuleta maendeleo.

“Siamini   kama  kuwaunga  mkono  wananchi  walionichagua yanatokana na tofauti za kisiasa kwani eneo hili linamilikiwa na Chama kimoja ambacho ni Chama cha Mapinduzi na wala sina  maslahi binafsi katika suala hilo,” alisema Makamba nakuongeza kuwa  yeye anawasimamia  wakulima wa zao la chai.

Kiwanda cha Mponde  kimefungwa  takribani  miezi  mitano  sasa kufuatia wakulima kususa kupeleka majani mabichi ya chai kwa madai ya kutaka uongozi wa Chama cha Wakulima wa Chai Usambara (UTEGA) uitishe Mkutano Mkuu kwa ajili ya kuwasomea mapato na matumizi.

Hivi karibuni Makamba, alimwaga machozi hadharani katika kijiji cha Mponde Kweminyasa kutokana na taarifa za watu watano kujeruhiwa kwa risasi za moto kutokana na vurugu zilizotokea kati ya wakulima wa zao la chai na Jeshi la polisi.

Vurugu hiyo ilitokea kutokana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Luteni Mstaafu Chiku Gallawa kuamuru kiwanda cha chai cha Mponde kilichokuwa kimefungwa kwa mwezi mmoja na nusu wakati  huo kifunguliwe kwa nguvu chini ya usimamizi wa Polisi jambo  ambalo zilisababisha vurugu kubwa mpaka watu kujeruhiwa  kwa  risasi za  moto.

No comments:

Post a Comment