Pages

Pages

Thursday, September 19, 2013

Dkt Kigoda awataka wananchi wa Handeni wabakishe mahindi ya chakula

Na Mashaka Mhando, Handeni
WAZIRI wa Viwanda na Biashara na Mbunge wa jimbo la Handeni Dk. Abdalah Kigoda amesema tabia ya wananchi wa jimbo hilo kuuza mahindi bila kuacha ziada ya chakula ndio inayosababisha wilaya hiyo kuomba chakula cha msaada mara kwa mara.

Dk. Kigoda aliyasema hayo wakati akiwa katika ziara ya kutembelea miradi kwenye kata zake pamoja na kupata taarifa ya kazi za chama na ya utekelezaji wa ilami ya Chama cha Mapunduzi (CCM).

"Wilaya ya Handeni ni ya kwanza kuzalisha mahindi, katika Mkoa wa Tanga, mahindi yetu yanauzwa ndadi na nje ya nchi,  lakini cha kushangaza sisi ndio wa kwanza kuathirika kwa njaa,” alisema.
Dk.Kigoda alisema Wilaya hiyo ni mioongoni mwa Wilaya za Mkoa wa Tanga zenye ardhi nzuri kwa ajili ya kilimo na wakulima wamekuwa wakivuna kwa kiwango kikubwa na kuuza mazao yao bila kujali kuweka akiba na hatimaye kujisababishia njaa.

Akiwa katika kijiji cha Gendagenda kata ya Mgambo Dk Kigoda alitembelea bwawa la maji lililopo kijijini hapo na kukutana na maombi ya wananchi ya kutaka kupatiwa madawa ya kutibu maji ya Bwawa hilo wanayoyatumia kwa ajili ya kunywa na matumizi mengine kama njia ya kujikinga na magonjwa ya kuhara.

Licha ya wakazi hao kusifu mbunge wao, Dk. Abdalah Kigoda kwa jitihada zake za kuwaletea wafadhili wa kujenga mabwawa ya maji katika eneo hilo wamesema ni vyema wakasaidiwa na dawa ya kuuliaa vimelea vya vijidudu.

Wakazi hao walisema kabla maji hayajapungua katika bwawa hilo kutokana na ukame, walikuwa wakiyatumia maji hayo bila madhara lakini yameanza kubadilika rangi hali ambayo inaashiria huenda yakawa na madhara kwa afya zao.

Mbunge wa jimbo hilo licha ya kuwashauri kuchemsha maji hayo alisema ifikapo mwaka 2015 miradi yote ya maji katika Jimbo hilo itakuwa imekamilika ili kuwaondosha wananchi na kero ya muda mrefu ya ukosefu wa maji safi na salama.

No comments:

Post a Comment