Pages

Pages

Thursday, August 01, 2013

Watoto waandaliwa shoo maalum ya kujiachia Idd Mosi

Kampuni ya Glitz Entertainment imeandaa Toto Party kwa ajili ya watoto wa jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake linayotarajiwa kufanyika katika Art Gallery iliyopo Mbezi Beach siku ya Iddi Mosi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam muandaaji wa tamasha hilo, Deniss Ssebo alisema kuwa hii ni mara ya nne kuandaa TOTO PARTY kwa ajili ya watoto, na wanatarajia kuanza kulipeleka na mikoani.

Katika Tamasha hilo, watoto watapata nafasi ya kushiriki katika michezo mbalimbali kama soka, kuogelea, kusaka hazina (Treasure hunt) na kujipaka rangi usoni (Face painting) na mengine mengi.

Aidha watoto hao pia wataweza kukutana na wenzao wanaoishi katika mazingira magumu.

Mbali na watoto kucheza na kufurahi michezo mbalimbali pia wazazi wao watachuana katika mchezo wa kuvuta kamba ambapo washindi katika michezo hiyo watazawadiwa zawadi mbalimbali na viingilio ni Sh 3,000 kwa watoto na wakubwa Sh 7,000.

No comments:

Post a Comment