Pages

Pages

Tuesday, August 06, 2013

Timu ya 3Pillars yaruhusiwa kucheza mechi za kirafiki Tanzania

TIMU ya 3Pillars Football Club ya Nigeria sasa inaruhusiwa kucheza mechi za kirafiki nchini baada ya kupata idhini ya Shirikisho la Mpira wa Miguu la Nigeria (NFF).

Msemaji wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Boniface Wambura, alisema kuwa awali tuliikatalia timu hiyo kucheza mechi za kirafiki nchini kwa vile haikuwa na barua kutoka NFF, lakini sasa Shirikisho hilo limetoa idhini hiyo. 

Pia ziara yake haikuwa inaratibiwa na wakala wa mechi anayetambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) au mwanachama wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Klabu hiyo kutoka Jimbo la Lagos ilipanga ziara hiyo kwa kuwasiliana na chama cha mpira wa miguu cha jimbo hilo ambacho nacho kilitakiwa kuomba idhini NFF kwa niaba ya 3Pillars.

Hivyo timu hiyo inaweza kucheza mechi, kwani ziara hiyo sasa inaratibiwa na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) ambaye ni mwanachama wetu.

Tunapenda kukumbusha kuwa watu pekee wanaotakiwa kuandaa mechi za kirafiki za kimataifa ni mawakala wa mechi wanaotambuliwa na FIFA au wanachama wa TFF.

No comments:

Post a Comment