Pages

Pages

Monday, August 26, 2013

Miss Utalii yasimamishwa, waandaaji watangaza kujipanga upya



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BODI ya Miss Utalii Tanzania, imetangaza kusimamisha kufanyika kwa mashindano hayo katika kipidi cha mwaka 2013/2014, lengo likiwa ni kujipanga upya na kuboresha mfumo wa uendeshaji na
usimamizi wa ngazi zote.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Rais wa Miss Utalii Tanzania, Gideon Chipungahelo, alisema kuwa uamuzi huo ni mgumu kuchukuliwa na bodi ya mashindano hayo yenye kuheshimika katika viunga mbalimbali vya nchi hii.

Alisema kuwa uamuzi huo umefikiwa baada ya kikao cha tathimini ya mashindano hayo tangu kuasisiwa kwake, huku akiamini kuwa kwa kusimamisha kwa kipindi kifupi, wadau wote watakaa chini kuangalia changamoto zinazowakabili.

“Fainali za kwanza za Miss Utalii Tanzania zilifanyika mwaka 2004 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam,  ambapo hapo historia ya Utalii ilianzishwa, hivyo tunaamini hizi ni changamoto tunazoangalia kwa kina,” alisema Chipungahelo.

Kwa mujibu wa Chipungahelo, bodi katika tathimini hiyo ya ndani imebaini changamoto mbalimbali za kimfumo, udhamini, utendaji, kuporomoka au kudumaa kwa sanaa ya urembo nchini, yakiwamo mashindano yao ya Miss Utalii Tanzania.

No comments:

Post a Comment