Pages

Pages

Sunday, August 11, 2013

Mapacha Watatu wajigamba kwa shoo ya nguvu ya utambulisho wa nyimbo zao mpya Agosti 16 Mzalendo Pub


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MMOJA wa Wakurugenzi wa bendi ya Mapacha Watatu, Khalid Chokoraa, amewataka mashabiki wao kuingia kwa wingi katika utambulisho wa nyimbo zao mpya katika Ukumbi wa Mzalendo Pub, Kijitonyama, jijini9 Dar es Salaam Agosti 16 mwaka huu.
Mapacha Watatu, pichani
Mbali na Mapacha Watatu, shoo hiyo pia itatumiwa na mwimbaji Ally Nipishe kutambulisha wimbo wake mpya wa Nikupulike katika ukumbi huo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, mmoja wa waandaaji wa shoo hiyo, Chokoraa, alisema kuwa maandalizi yamekamilika kwa bendi hiyo kufanya tukio kubwa la kiburudani.

Alisema nyimbo za Mapacha Watatu ni ‘Kisu cha Kuokota’, ‘Furaha’ na ‘Sauti ya Marehemu’, huku akiamini kuwa mashabiki wao watapata kitu adimu kutoka kwenye onyesho hilo.

“Hii ni shoo ya aina yake itakayofanyika katika Ukumbi huo, ambapo Mapacha Watatu na Ally Nipishe watatoa burudani za aina yake kwa wadau na mashabiki wao,” alisema.

Mapacha Watatu inaundwa na wakali Khalid Chokoraa na Jose Mara, huku Nipishe naye akiibukia kwa kasi katika anga la muziki wa kizazi kipya, maarufu kama Bongo Fleva.


No comments:

Post a Comment