Pages

Pages

Saturday, August 31, 2013

Dayna ashusha pumzi

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
NYOTA wa muziki wa kizazi kipya, Mwanaisha Said maarufu kama ‘Dayna’, amesema yupo katika nafasi nzuri kisanaa kutokana na kudhamiria kufanya makubwa katika sanaa hiyo na kuwapa raha mashabiki wanaomuunga mkono.
Dayna akiwa amepozi kama unavyomuona hapo.
Mwimbaji huyo wa ‘Mafungu ya Nyanya’ aliliambia gazeti hili juzi jijini Dar es Salaam kuwa mpaka sasa ameweza kuachia nyimbo tatu ambazo zote zilipokelewa kwa shangwe.

Alisema hali hiyo inamfanya aamini kuwa kiwango chake kimuziki kimefikia sehemu nzuri kiasi cha kumpa imani ya kuendelea kuwa juu katika tasnia hiyo.

“Nilianza na wimbo wangu wa Mafungu ya Nyanya na kufuatiwa na nyimbo mbili makini na zilizokonga nyoyo za mashabiki wangu kila nilipotia mguu.

“Najisikia vizuri katika hilo, ndio maana nyimbo zangu za Fimbo ya Mapenzi na Nivute Kwako zote ziliwafurahisha wadau na mashabiki wangu kimuziki,” alisema Dayna.

Wimbo wake wa Mafungu ya Nyanya aliimba na msanii Lawrence Malima maarufu kwa jina la ‘Marlaw’ msanii aliyekuwa kimya kwa sasa baada ya kutamba miaka kadhaa iliyopita.

No comments:

Post a Comment