Pages

Pages

Monday, August 26, 2013

CCM yafanya maamuzi magumu ya kumvua uanachama Mansoor Yussuf Himid


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyomalizika leo imejadili kwa kina Masuala mbalimbali likiwemo pendekezo la Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Magharibi - Zanzibar la kumvua uanachama Ndugu Mansoor Yussuf Himid (pichani), Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Kiembesamaki.

Baadhi ya tuhuma za Ndugu Mansoor Yussuf Himid ni pamoja na:-

1.   Kushindwa kusimamia malengo ya CCM na kutekeleza masharti ya uanachama.

2.   Kushindwa kutekeleza wajibu wa mwanachama na kukiuka Maadili ya Kiongozi wa CCM.

3.   Kuikana Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010-2015 na kuisaliti CCM.

Baada ya kujiridhisha vya kutosha na tuhuma dhidi ya Ndugu Mansoor Yussuf Himid, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) imeridhia uamuzi wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Magharibi Zanzibar wa kumfukuza uanachama. Kwa uamuzi huo wa kumvua uanachama wa CCM Ndugu Mansoor Yussuf Himid, yeye kwa sasa sio Kiongozi tena wa CCM.

Imetolewa na:

Nape Moses Nnauye,
KATIBU
WA NEC ITIKADI NA UENEZI CCM TAIFA
26/08/2013

No comments:

Post a Comment