Pages

Pages

Sunday, August 04, 2013

Bondia Japhet Kaseba aendelea kusifia makali yake Tanzania



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BONDIA wa Ngumi za kulipwa hapa nchini, Japhet Kaseba, amesema kwamba makali yake yanamfanya aone anaweza kucheza na bondia yoyote mwenye kujitapa kuwa ana kiwango cha juu katika masumbwi hapa nchini.

Kaseba ameyasema hayo huku akifanikiwa kuingiza sokoni filamu yake ya mapigano iliyokwenda kwa jina la Bongo Mafia iliyoshirikisha wacheza filamu wengi wenye majina makubwa hapa nchini.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Kaseba alisema kuwa kila siku amekuwa akitenga muda mrefu kufanya mazoezi kwa ajili ya kulinda kiwango chake kinachoogopesha mabondia wengi hapa nchini.

“Mchezo wa ngumi unafikia wakati na kuona sasa una uwezo wa kucheza na mtu yoyote, hivyo nadhani kwa makali yangu ni makubwa na ndio maana mabondia wengi wamekuwa wakipata woga wa kupanda ulingoni kucheza na mimi.

“Naamini nitaendelea kuwa juu katika masumbwi kwa kuhakikisha kuwa najiweka vizuri muda wote, ukizingatia kuwa nimeamua kujikita moja kwa moja katika mchezo wa masumbwi kwakuwa ndio vitu ninavyopenda,” alisema Kaseba.

Kaseba ni miongoni mwa mabondia wenye uzito wa juu, huku akiwahi kutamba pia katika mchezo wa Kick Boxing ambapo aliwahi kutwaa Ubingwa wa Dunia wa ngumi za mateke na kuweka rekodi kimatafa.
Mwisho

No comments:

Post a Comment