Pages

Pages

Thursday, August 15, 2013

Benki ya CRDB yatangaza neema ya mkopo wa nyumba kwa wateja wao

Mkugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei, akizungumza na wadau mbalimbali katika akizindua Mikopo ya nyumba ijulikanayo kwa jina la Jijenge itakayotolewa na benki hiyo, Dar es Salaam jana.

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WATEJA wa benki ya CRDB na Watanzania kwa ujumla, sasa wanaweza kupata nyumba kwa urahisi, endapo wataamua kujiunga na huduma mpya ya Jijenge iliyozinduliwa jana jijini Dar es Salaam.

Katika huduma hiyo mpya, mteja wa CRDB anaweza kukopa fedha za kujenga nyumba ya kisasa, kukarabati au kununua na kutakiwa kulipa katika kipindi cha miaka 20.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dk Charles Kimei, alisema wameamua kuanzisha huduma hiyo ili kuwakomboa Watanzania katika kipindi cha ukosefu wa nyumba bora za kuishi.

Alisema kuwa Watanzania wengi wamekuwa na changamoto za kukosa makazi bora ya kuishi, hivyo yoyote anaweza kuchukua mkopo wa kununua nyumba, kujenga au kukarabati na kutakiwa alipe katika kipindi cha miaka 20.

“Hii ni hatua ya CRDB kuboresha makazi ya Watanzania wote, ukizingatia kuwa kumiliki nyumba kwa Dunia ya leo ni mtihani mkubwa kutokana na ugumu wa maisha.

“Kinachotakiwa ni kufika kwa tawi lolote la CRDB na kuonyesha kiwango cha mshahara wako, huku mtu kuanzia mwenye mshahara kuanzia 200,000 akiwa na sifa ya kupata mkopo,” alisema.

Aidha, Kimei alisema sio waajiriwa tu, ila hata wajasiriamali nao wanaweza kupata mkopo huo ambao umeanzishwa kwa ajili ya kuboresha makazi ya Watanzania wote.

No comments:

Post a Comment