Pages

Pages

Wednesday, August 28, 2013

Ally Nipishe kufanya mambo Face Pub Ijumaa


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Ally Nipishe, anatarajia kufanya shoo ya aina yake katika uzinduzi wa disco la Crazy Night, linalotarajiwa kufanyika Ijumaa hii, katika Ukumbi wa Face Pub, Tabata, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Nipishe alisema kwamba amejipanga imara kuhakikisha kuwa anafanya vitu vya aina yake katika usiku huo wa burudani Tabata, jijini Dar es Salaam.

Alisema kuwa lengo lake ni kuwapa burudani kamili mashabiki wake wa Tabata na vitongoji vyake, hivyo wadau wajitokeze kwa wingi kupata burudani.

“Nimejipanga imara kuhakikisha kuwa natoaa burudani kabambe kwa mashabiki wangu wa muziki wa kizazi kipya katikaa uzinduzi wa disco la Crazy Night.


“Naamini kila atakayeingia katika ukumbi huo atapata vitu adimu kutoka kwangu, ukizingatia kuwa lengo langu ni kuwapatia burudani,” alisema.

Nipishe ni miongoni mwa wasanii wanaoibukia kwa kasi, huku akipangwa kufanya shoo katika usiku huo wa aina yake.

No comments:

Post a Comment