Pages

Pages

Wednesday, July 24, 2013

Simba wahaha kuongeza wa kuboresha kikosi chao


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Pope, amesema kwamba bado kunahitajika beki na mshambuliaji ili kuifanya klabu yao iwe na uhakika wa kufanya vizuri katika michuano ijayo.
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage
Katika mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya URA ya nchini Uganda, Simba walifungwa bao 2-1 na kuleta majonzi kwa mashabiki wao.

Akizungumza mwishoni mwa wiki, Hans Pope alisema kuwa bado kuna umuhimu wa kuongeza wachezaji kwa ajili ya kuifanya timu yao iweze kufanya vizuri katika michuano ijayo, ikiwamo Ligi ya Tanzania Bara.

Alisema japo wachezaji waliocheza mechi dhidi ya URA wanaonyesha kiwango, ila wakiongeza nguvu kulingana na mapengo yanayoonekana, mambo yatakuwa mazuri.

“Tunahitaji kuwa na kikosi  imara kwa ajili ya kuwapa shangwe mashabiki wetu, hivyo tunakusudia kuendelea kutafuta wachezaji kadhaa kabla ya ligi kuanza.

“Tumeona wote bado kuna nafasi zinahitajika, ikiwamo beki bora na mshambuliaji kabla ya ligi kuanza, ukizingatia kuwa tunataka tufanye vyema katika michuano itakayoanza Agosti 24 mwaka huu,” alisema.

Ligi ya Tanzania Bara inatarajiwa kuanza Agosti 24 mwaka huu kwa kushirikisha timu 14 ambazo zimeanza mazoezi kwa ajili ya patashika hiyo.

No comments:

Post a Comment