Pages

Pages

Saturday, July 06, 2013

Big aikumbuka filamu ya Masaa 24 na kusema haijawahi kutokea



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
NYOTA wa filamu hapa nchini, Lumolwe Matovolwa ‘Big’  amesema kuwa haamini kama kuna siku Tanzania itaandaliwa filamu nzuri zaidi ya Masaa 24, iliyotokea kuwa gumzo katika tasnia hiyo.
          Msanii Big akiwa amejiachia kama unavyomuona.
Filamu hiyo ilikusanya wasanii mahiri, akiwamo Big mwenyewe, Dk Cheni, Haji Adam, ambapo ilikuwa ikielezea kwa kina sekeseke la mapenzi ya kweli na usaliti ndani yake.

Akizungumza mapema wiki iliyopita, Big alisema kuwa filamu ya Masaa 24 iliweza kuwa tishio katika tasnia hiyo na kupendwa na kila mmoja, ikiwa ni kutokana na uandaaji wake uliokuwa na kiwango cha juu.

Alisema zipo filamu nyingi nzuri, ila kazi hiyo iliyotoka miaka ya 2“Nimewahi kuona ama kucheza filamu nyingi nzuri, ila Masaa 24 ilikuwa juu zaidi, ndio maana bado naikumbuka kwa kiasi kikubwa, sambamba na jinsi wasanii walivyoweza kuonyesha uwezo wao.

“Hii inanifanya wakati mwingine nitamani kuiangalia tena, ingawa mimi ni miongoni mwa wale walioifanikisha kuingia sokoni na kudhihirisha kuwa Watanzania wanaweza kufanya sanaa hii,” alisema Big.

Msanii huyo anaheshimika sana katika sanaa ya maigizo na filamu, akicheza filamu mbalimbali, ikiwamo ya Masaa 24, Mtaani Kwetu na nyinginezo, huku akiwa ni mwenyekiti wa Tawi la Yanga la Green Stone, lenye maskani yake Mwananyamala, jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment