Pages

Pages

Friday, June 14, 2013

Wasanii wawili wafariki Dunia jana jioni akiwapo Langa Kileo na kuendeleza wimbi la vifo vyao, baada ya kuzikwa Ngwair Morogoro



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
ALHAMISI ya jana, itakuwa chungu kwa sanaa na wasanii baada ya kutokea vifo viwili vya wasanii, akiwapo mwimbaji wa Hip Hop, Langa Kileo na mcheza filamu wa Bongo Movie, Hassan Kihiyo.
                     Marehemu Langa Kileo enzi za uhai wake
Vifo vyote hivyo vilitokea jana, baada ya kulazwa katika Hospitali walipokuwa wakitibiwa na kusababisha vifo vyao na kuleta majonzi makubwa katika sanaa Tanzania.
Marehemu Ngwair aliyezikwa mkoani Morogoro wiki iliyopita na kuzua balaa kubwa kwa mashabiki wake.

Marehemu Kihiyo anatarajiwa kuzikwa leo jioni katika makaburi ya Mwinyimkuu Magomeni, jijini Dar es Salaam, wakati Langa yeye atazikwa Jumatatu, katika makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Msanii wa maigizo Kash aliyezikwa mapema wiki hii.
Wadau mbalimbali wamekuwa na maoni tofauti juu ya mwendelezo wa vifo hivyo, ukizingatia kuwa vimetokea siku chache baada ya kuzikwa Albert Mangweha ‘Ngwair’ na mwanadada Kash msanii wa maigizo aliyezikwa mapema wiki hii.

Msanii nguli na mtunzi wa filamu Tanzania, Muddy Kimindu Kulinyangwa, aliiambia Handeni Kwetu kuwa Kihiyo ni miongoni mwa wasanii wenye mchango mkubwa katika sanaa.

Msemaji wa Hospitali ya Muhimbili, Aminiel Aligaesha, aliimbia Handeni Kwetu jana jioni kuwa chanzo cha msiba wa Langa kitajulikana baada ya ripoti kutolewa na daktari wake, ingawa habari zilizobuka pia zinasema msanii huyo wa Hip Hop alikuwa na malaria kali.

Ratiba juu ya msiba wa Langa imetoka, huku ukiwa nyumbani kwao Mikocheni, ambapo Jumatatu utazikwa baada ya tukio la kumuaga likikamilika.

Hata hivyo, wapo waliozidisha makali juu ya kifo cha Langa kwa kukihusisha moja kwa moja na matumizi mabaya ya dawa za kulevya, ambapo msanii huyo alikuwa akitumia kabla ya kuumanisha umma kuwa ameacha ulaji huo wa dawa za kulevya.

Langa ni miongoni mwa wasanii wa Tanzania waliokuwa wamejiingiza katika vitendo vibaya vya uvutaji huo wa dawa za kulevya, jambo lillosababisha pia umaarufu wao na uwezo wao kisanaa kuchuka kama sio kwisha kabisa.

Langa aliibuka katika kundi la Wakilisha, likiwa na wasanii watatu, Sara, Witness nay eye mwenyewe, ambapo walichomoza baada ya kushinda shindano la Coca Cola Pop Stars nchini Afrika Kusini.

Nyimbo zilizoimbwa na kufanya vizuri ni pamoja na Swanglish, Matawi ya Juu, pamoja na nyimbo nyingi alizoshirikishwa ukiwapo ule wa Chagua Moja wa Fid Q.

No comments:

Post a Comment