Pages

Pages

Saturday, June 15, 2013

Timu ya vijana ya Coastal Union yaanza kujinoa



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
TIMU B ya Coastal Union yenye maskani yake jijini Tanga, imeanza mazoezi rasmi kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya Rolling Stone yatakayofanyika jijini Arusha baadaye mwezi ujao.

Vijana wa timu B ya Coastal Union wakijinoa uwanjani.
Mashindano yaliyopita yalifanyika nchini Burundi, huku vijana hao wakifanikiwa kushika nafasi ya pili na kulitangaza vyema Taifa katika michuano ya vijana.

Akizungumza na Handeni Kwetu, Meneja wa timu hiyo ya vijana, Abdulrahaman Ubinde, alisema vijana wake wameanza mazoezi huku wakiwa na malengo katika mashindano hayo.

Alisema timu yao ya vijana inafanya mazoezi kabambe kwa ajili ya kujiweka sawa kwa ajili ya mashindano hayo ya Rolling Stone yenye ushindani wa aina yake kwa mpira wa miguu.

 “Tunatarajia uwezo wa kutosha katika mashindano hayo ya Rolling Stone ambayo kwa hakika yamekuwa na ushindani wa aina yake, huku mwaka jana tukishika naafsi ya pili.

 “Vijana wapo Tanga wakiendelea na mazoezi makali kwa ajili ya kujiandaa na mashindano haya, huku tukiamini kuwa mambo yetu yatakuwa mazuri zaidi msimu huu,” alisema Ubinde.

Coastal Union ni miongoni mwa timu zenye malengo ya yake katika mpira wa miguu, huku ikijipanga zaidi katika soka la vijana kama njia ya kuzalisha wachezaji wenye uwezo wa kutosha.

Xxxx

No comments:

Post a Comment