Pages

Pages

Monday, June 03, 2013

Siasa mkoani Tabora zapamba moto, kada wa CCM akanusha kutuma watu wamzomee mbunge Aden Rage



Na Mwandishi Wetu, Tabora
KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Tabora na mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Wilaya, Emmanuel Mwakasaka, pichani juu, amekanusha vikali tuhuma za baadhi ya wanachama na viongozi wa CCM kuwa aliwapa vijana fedha ili wamzomee mbunge wa jimbo la Tabora mjini, Ismail Aden Rage.

Mbunge wa Tabora Mjini, Ismail Aden Rage
Mapema siku ya jumamosi ya mwezi mei 25 mwaka huu,chama cha
mapinduzi,(CCM),mkoa wa Tabora walifanya mkutano wa hadhara kwenye
viwanja vya stendi ya mabasi zamani ambapo kuliibuka zomea zomea toka
kwa wananchi.

Aidha wananchi hao walipokuwa wakizomea walisikika wakitamka kuwa
wamechoka na propaganda wanachotaka ni barabara za
lami,Tabora-Nzega,Tabora-Urambo na ile ya Itigi-Tabora.
Hata hivyo baada ya siku kadhaa yameibuka maneno ya chini chini
yakimtuhumu kada wa CCM Emmanuel Mwakasaka ndiye aliyekuwa nyuma ya zomeazomea hiyo akidaiwa aliwapa vijana kadhaa fedha ili wamzomee Aden Rage mbunge wa Tabora mjini.

Hali ilimfanya Mwakasaka ambaye pia ni mlezi wa chipukizi na mjumbe wa
kamati ya uchumi mkoa wa Tabora, kulazimika kuongea na waandishi wa
habari na kukanusha na kufafanua juu ya taarifa hizo.

Mwakasaka alisema kamwe kama kada wa CCM hawezi kufanya kitu cha namna hiyo na kwamba kujitoa katika misaada mbalimbali kwa chama chake ndiyo chanzo kikuu ya kuchafuliwa jina lake.

“Nimekuwa nikitoa misaada mingi kwa chama changu na nimekuwa
nikisaidia jumuiya zote za chama za UWT, UVCCM na WAZAZI na kila
ninapotoa misaada nimekuwa nikipatiwa barua ya shukrani na risiti sasa
leo mimi ninachafuliwa jina langu eti nilituma watu wamzomee mbunge
inaingia akilini kweli,” alishangazwa.

Alisema kamwe hawezi kumpiga vita mbunge kwa sababu ya kutaka ubunge na zaidi muda wa ubunge bado na taratibu za chama zinaeleweka kama atahitaji ubunge atatangaza lakini siyo kweli anampiga vita mbunge wa jimbo la Tabora mjini Aden Rage.

Alisema imemuumiza sana tetesi hizo na kama angetuma vijana kumzomea
Rage na asingeweza kumchangia siku kiasi cha sh 100,000 za kumuunga
mkono kwenye miradi aliyoitekeleza kwenye jimbo lake.

“Ufadhili kwa chama changu ndiko kunakoniponza kwa watu wachache ndani ya chama hawafurahishwi na hali hiyo kwa maslahi yao binafsi…..chuki zinaanzishwa na wapambe wachache ili kumdhoofisha na kumchonganisha na Rage kamwe mtego huo hawezi kuingia,”alisema.

Alisema ana imani kubwa na Rage kama mbunge na kwamba ataendelea
kumchangia kwenye miradi ambayo anatekeleza ilani ya chama chao kitajengwa kwa kushirikiana kwa watu wote.

Aliongeza kuwa nayofanya kama kutoa misaada ni katika kumuunga mkono mbunge wetu na chama ili kuhakikisha wananchi wanatuunga mkono katika kuwakomboa.

Alimalizia kwa kusema haamini katika uhalisia wa kawaida kama wana CCM wanaweza fikia mahali wakazusha jambo la namna hiyo ili kumchonganisha na Rage, uongozi wa chama mkoa na taifa.

No comments:

Post a Comment